Kamati ya ulinzi na usalama
wilayani Mkinga imebaini kuwepo kwa kisiwa maalum cha maficho ya
wahamiaji haramu kutoka Somalia na Ethiopia ambapo wametengeneza
kiwanja maalum ndani ya kisiwa hicho kwa ajili ya kufanya mazoezi.
Kisiwa hicho kinachojulikana kwa
jina la Kirui chenye ukubwa wa hekta 600 kilichopo katika bahari ya
hindi kimeanza kuleta hofu kwa Kamati hiyo ambapo askari waliokuwa na
silaha mbali mbali walilazimika kuvamia kisiwa hicho kwa muda wa siku
mbili na kufanikiwa Kukamata wahamiaji haramu kutoka Ethiopia na
Somalia wapatao 22 huku wengine wakidaiwa kutoroka ndani ya kichaka cha
msitu huo wa miti aina ya mikoko.
Kwa upande wake afisa misitu
wilayani Mkinga bwana Frank Chambo amesema akielezea uharibifu
uliofanywa na baadhi ya watu Kutoka nchini Kenya amesema wamebaini
kuwepo kwa shehena ya magogo pamoja na mbao baada ya kuazisha viwanda
vidogo ndani ya hifadhi hiyo.
Kufuatia hatua hiyo afisa
uhamiaji mkoani Tanga bwana Sixtus nyaki amesema idara yake imeanza
kufanya utaratibu wa kuwachukulia hatua kali za kisheria ikiwa ni pamoja
na kutumikia kifungo kisha kuwarejesha nchini mwao lakini taarifa
walizonazo lipo kundi kubwa la wahamiaji kutoka nchi mbali mbali na hivi
sasa wanaandaa utaratibu ili kuvamia ndani ya pori
hilo.
-ITV