Katika azimio lao viongozi wa Afrika wamesema kuwa kiongozi yeyote wa taifa hatatakiwa kuhudhuria mahakama yoyote ya kimataifa wakati yuko madarakani.
Viongozi hao wamefikia maazimio hayo baada ya kuishutumu ICC kuwa na kigeugeu – kwamba inawashtaki Waafrika na siyo watu wa mataifa ya magharibi.
Mkutano huo umekusudia kuwatuma Marais watano wa Afrika nchini Uholanzi ili kuitaka Mahakama hiyo kuahirisha kesi ya rais Kenyatta itakayoanza November 12 ambapo pia mkutano huu umesema hata Naibu Rais William Ruto hafai kushtakiwa kwenye Mahakama hiyo ya ICC.