1. Nchini China kumuua mnyama aina ya Panda ni kosa ambalo adhabu yake ni hukumu ya kifo.
2. Ubongo wa mwanadamu hutumia asilimia 25 ya nguvu za mwili
3. Nchini Iran asilimia 70 ya wanafunzi wanaochukua masomo ya uhandisi ni wanawake tofauti na nchi Za Afrika ambazo wanaume ndio wengi wanaosoma uhandisi kuliko wanawake.
4. Kuna kundi la nyani wanaoitwa Bonobo, hawa nyani husalimiana kwa kufanya ngono.
5. Ngamia ana uwezo wa kunywa maji ya wingi wa galoni 30 ambazo ni sawa na na lita 113 ndai ya muda wa dakika 13 pekee.
6. Mnyama aina ya Twiga anaweza kusafisha masikio yake kwa kutumia ulimi wake ambao una urefu wa nchi 21.
7. Mwaka 2003 kijana mdogo Mark Zuckerberg alitengeneza mtandao wa facemash ambao ulikuwa mtandao wa kutuma picha za wanafunzi wenzie ambao alikuwa na lengo la kufahamu ni mwanafunzi gani ana mvuto kuliko mwenzie, leo hii mtandao huu ni facebook ambao umekuwa mtandao wa kijamii mkubwa kuliko yote duniani.
8. Mwaka 1619 wakulima nchini Marekani walikuwa wanalazimishwa na sheria za majimbo yao kulima mmea wa bangi.
-millardayo