MAPENZI
ni maisha rafiki zangu. Kama kuna kitu kinachohitaji kufanyiwa uamuzi
sahihi zaidi maishani basi ni mapenzi. Ukifanya makosa katika eneo hili,
mambo yako mengi yatakuwa ya kuyumba tu!
Ipo
mifano mingi sana. Mathalani mtu mwenye uhusiano kwa zaidi ya mwenzi
mmoja, mara nyingi huyumba kimaisha, hata kwenye kufanya uamuzi wa mambo
yake mbalimbali.
Huu ndiyo ukweli ambao wengi hawapendi kuusikia. Nimesema hayo kama utangulizi 2.
Mada
inayosomeka hapo juu, imezalishwa na maswali mengi kutoka kwa wadau
mbalimbali waliotaka kujua namna ya ama kuishi vyema na wenzi walio
kwenye ndoa, namna ya kutoka katika kifungo hicho huku wengine wakiwa
hawajui cha kufanya.
Kwa
nyakati tofauti, simu yangu iliingiza ujumbe mfupi wa maneno kila mmoja
akiwa na matatizo yake, lakini yenye mlengo sawa. Hapa nitachapa sms
tatu tu kati ya hizo, ninaamini zitakupa mwanga wa wapi pa kuanzia...
MSOMAJI WA KWANZA:
“Nashukuru
sana kaka Shaluwa kwa namna unavyotusaidia kwenye uhusiano wetu. Kwa
kweli unahitaji pongezi. Kaka yangu, nina tatizo. Nipo kwenye uhusiano
na mwanaume mmoja hivi, kwa miaka mitatu sasa. Nampenda sana huyu
mwanaume.
“Kitu
cha kushangaza ni kwamba, kwa muda wote ambao nimekuwa naye, hatujawahi
kuzungumzia kabisa suala la kuoana. Juzi tu, nimegundua kitu
kilichonishtua sana. Kumbe jamaa ni mume wa mtu na amezaa na mke wake
watoto watatu.
“Ni
jambo lililoniumiza sana, nilipojaribu kumwuliza, hakukataa lakini
aliniomba msamaha kwa kutonieleza ukweli mapema. Yote tisa, kumi ni
kwamba nampenda sana na siwezi kumuacha. Je, nifanyeje kaka yangu?”
MSOMAJI WA PILI:
“Kuna
jamaa nimetokea kumpenda sana, lakini nimegundua ni mume wa mtu. Je,
nitumie mbinu gani ili nimpate? Naomba msaada wako katika hili.”
MSOMAJI WA TATU:
“Nimekuwa
katika uhusiano na mke wa mtu kwa miaka miwili sasa. Tunapendana sana
kwa kweli na yeye mwenyewe amesema hawezi kuniacha. Tatizo ni kwamba,
mume wake ameanza kuhisi mabadiliko ya mkewe. Nifanyeje ili kuinusuru
ndoa ya mpenzi wangu na wakati huo huo penzi letu likiendelea?”
UMEJIFUNZA NINI?
Wewe
umepata nini kupitia meseji hizo hapo juu? Kwamba mwingine yupo kwenye
uhusiano na mume wa mtu na amegundua, anataka msaada lakini hana mpango
wa kumuacha.
Yupo
ambaye anatembea na mke wa mtu na anafahamu wazi kuwa aliyenaye ni
‘mali’ za watu, lakini anaomba msaada wa namna ya kuendelea naye huku
ndoa yake ikiwa salama.
Mwingine
anasema, amempenda mume wa mtu, anachohitaji ni mbinu za kumtokea.
Umeona hapo? Hakuna mwenye mpango wa kuacha hata kama amegundua kuwa
aliyenaye ana mwenyewe tena halali kabisa, pengine kisheria au kidini.
WEWE UKOJE?
Siku
za hivi karibuni kumekuwa na mtindo wa watu kutoka na wake/waume za
watu. Tatizo hili lipo zaidi kwa wanawake. Bila aibu huku akijua kuwa
mwanaume aliyenaye ni mume wa mtu anatembea naye. Wengine wanatamba
kwamba wao ni washindi.
Kwamba
wake zao hawana lolote, ndiyo maana wakakimbilia nje na kufanikiwa
kuwanasa. Hizi ni tambo za kijinga. Hakuna usahihi wowote wa mtu
kutembea na ‘mali’ za watu.
Je,
wewe unayesoma mada hii ukoje? Ni mke wa mtu lakini una mwanaume
mwingine wa pembeni? Ni mume wa mtu, lakini una kimada wako wa nje? Kuna
mke wa mtu anakutega kimapenzi au mume wa mtu anakusumbua akikutaka?
Uko
kundi gani? Kujua ulipo, angalau kutakupa nafasi ya kuingia katika
kipengele cha pili, ambacho ni kujifunza juu ya yote hayo. Rafiki zangu,
najua kuna baadhi yenu hampendi ninachokiandika hapa lakini ni tatizo
kubwa kwa wengine.
Ikiwa
utaweka ubongo wako tayari kujifunza, kuna kitu utakipata kupitia mada
hii. Zipo athari unazoweza kuzipata ukiwa katika uhusiano na mke/mume wa
mtu. Hebu tuendelee kujifunza.
Siku za hivi
karibuni kumekuwa na mtindo wa watu kutoka na wake/waume za watu. Tatizo
hili lipo zaidi kwa wanawake. Bila aibu huku akijua kuwa mwanaume
aliyenaye ni mume wa mtu anatembea naye. Wengine wanatamba kwamba wao ni
washindi.
Kwamba wake zao hawana lolote, ndiyo maana wakakimbilia nje na kufanikiwa kuwanasa. Hizi ni tambo za kijinga. Hakuna usahihi wowote wa mtu kutembea na ‘mali’ za watu.
Je, wewe unayesoma mada hii ukoje? Ni mke wa mtu lakini una mwanaume mwingine wa pembeni? Ni mume wa mtu, lakini una kimada wako wa nje? Kuna mke wa mtu anakutega kimapenzi au mume wa mtu anakusumbua akikutaka?
Uko kundi gani? Kujua ulipo, angalau kutakupa nafasi ya kuingia katika kipengele cha pili, ambacho ni kujifunza juu ya yote hayo. Rafiki zangu, najua kuna baadhi yenu hampendi ninachokiandika hapa lakini ni tatizo kubwa kwa wengine.
Ikiwa utaweka ubongo wako tayari kujifunza, kuna kitu utakipata kupitia mada hii. Zipo athari unazoweza kuzipata ukiwa katika uhusiano na mke/mume wa mtu.
Athara kubwa ambayo unaweza kuipata pindi tu unapokua kwenye mahusiano na mke/mume wa mtu ni hiyo hapo chini... UNAPOTEZA MALENGO
Kwanza kabisa, hakuna malengo unayoweza kutengeneza na mke au mume wa mtu. Tayari mwenzako yupo kwenye ndoa yake, kwa hiyo kuwa naye hakuwezi kubadilisha matokeo (hasa kama ana ndoa ya mke mmoja).
Sana sana unapoteza muda wako na kuziba bahati ya kuingia katika ndoa yako peke yako. Huwezi kuwa na malengo yoyote kwa kuwa katika uhusiano na mtu mwenye ndoa yake.