Ufoo Saro wakati akitolewa chumba cha upasuaji kupelekwa wodini. |
Manesi wakimpeleka Ufoo wodini. Baadhi ya waandishi na wananchi wakiwa wamekusanyika katika Hospitali ya Taifa Muhimbili kujua hali ya Ufoo.
Mtangazaji wa ITV na Radio One, Ufoo Saro amefanyiwa upasuaji baada ya kujeruhiwa vibaya kwa risasi na mzazi mwenziye aitwaye Anther Mushi mapema leo. Upasuaji huo umefanyika katika Hospitali ya Taifa Muhimbili kuanzia asubuhi mpaka saa 12 jioni. Ufoo alipigwa risasi akiwa nyumbani kwa mama yake mzazi Annastazia Saro baada ya kutokea mgogoro baina yake na mzazi mwenziye. Katika tukio hilo, Anther alimpiga risasi na kumuua mama Ufoo kisha na yeye akajilipua kwa risasi baada ya kumpiga risasi Ufoo. Kwa sasa Ufoo amehamishiwa katika wodi ya Kibasila anapoendelea kupatiwa matibabu. Umati wa watu ulikusanyika katika Hospitali ya Taifa Muhimbili kuanzia asubuhi ili kujua hali ya mtangazaji huyo.