ITV ilifika nyumbani kwao marehemu Baraka
Deogratias ambaye ni mwanafunzi wa darasa la tatu katika shule ya msingi
Kitunda,na kukuta ndugu jamaa na marafiki wakiwa katika msiba
huo,ambapo mama mzazi wa marehemu Baraka Bi Veronica Jeremiah amesema
siku ya Jumamosi ya tarehe 5 Octoba 2013 saa 2 usiku mume wake bwana
Masaka Limbu alifika nyumbani na kuanza kukagua madaftari ya watoto
wawili ambao ni Pita masaka ambaye ni mtoto halali wa mtuhumiwa na
Baraka Deogratias ambaye ni mtoto wa kambo ...
Wakiwa chumbani na baba yao
alisikia kilio cha mtoto wake ambaye hakuzaliwa na mume huyo
akilia kwa uchungu lakini alipofika alikuta hajiwezi na alipomkimbiza
katika zahanati ya eneo hilo,mtoto alipoteza maisha huku baba halali wa
marehemu akionyesha kuumizwa na kifo cha mtoto wake.
Baadhi ya wazee wa eneo hilo wamemlalamikia
mtuhumiwa bwana Masaka Limbu,kwa tabia yake ya kupenda ugomvi na
kuongeza kuwa kuna adhabu zingine zinazidi mipaka katika kumwadhibu
mtoto huku mtoto mdogo aliyeshuhudia hali hiyo akisimulia.
Kamanda wa polisi mkoa wa kipolisi ilala Acp
Marietha Minangi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo huku mkurugenzi
mtendaji wa tamwa Bi Valerie Msoka ameionya jamii kuachana na
vitendo vya ukatili ndani ya jamii ambavyo vinasababisha madhara makubwa
na kugeuka kuwa majuto katika maisha yao.