Tumemsikia
Mwazani Said leo katika leo tena akituelezea namna alivyonusurika
katika ajali ya gari iliyopelekea wasanii 13 ya band ya taarab ya 5stars
kupoteza maisha.Ajali hiyo ilitokea tarehe 22 mwezi wa 3 mwaka
2011.Mwazani alisafiri na band kama mcheza show lakini yeye ilikuwa ni
mara ya kwanza.Rafiki yake ambae alikufa kwenye band ndio alimwambia
kuna kazi ya kucheza mikoani ambayo atatoka na pesa kidogo kuliko kukaa
bure.
Wakasafiri
na kuzuru mikoa mitano na yeye akafanya kazi yake ambayo alilipwa Tsh
100,000.Siku mbili kabla ya kurejea Dar wasanii waliopoteza maisha
walikuwa wakiona vitu vya mauza uza.Msanii Issa Kijoti na mwimbaji
mwingine wa kike walitokewa na mtu aliyevaa nguo nyeupe.Wakawaambia
wenzao juu ya hilo wakawafanyia kisomo na dua ili waweze kukaa sawa.
Pia
kulizuka ugomvi mkubwa ambao wasanii walikuwa wakigombana wao kwa wao
mpaka Sheba Juma ambae ni marehemu alitaka kuondoka mwenyewe kurudi
Dar.Lakini Ali J ambae yu hai alinusurika alisuluhisha ugomvi huo wakawa
sawa.
Katika
ajali hiyo wakiwa kwenye basi mwazani alikuwa amelala.Alikaa siti moja
na marehemu Sheba Juma akamuomba wabadilishane siti ili yeye Mwazani
alale maana alikuwa na usingizi.Alipolala alikuja kuzinduka baada ya
siku 5 na kujikuta yupo hospital mkono umepooza na mguu umefanyiwa
upasuaji na kuwekewa vyuma.Akamuuliza mama yake kumetokea nini mbona
yupo hospital mama hakumjibu.Baba ndio akamletea gazeti akasoma na kuona
kilichotokea na yule shosti wake aliyemuita wakacheze alipoteza maisha.
Baada
ya ajali ile mpaka sasa mkono wake wa kushoto umepooza na mguu wa
kushoto pia unavyuma bado.Walilipwa pesa ambazo yeye alizinunulia eneokanyumba kadogo kakuishi.
Wakati
ananunua hapa sio yeye alikuja kununua.Kuna ndugu yake alikuja
kupanunua lakini hakukuwa na choo.Ni mwaka sasa amekuwa akitumia choo
cha jirani na kwa sasa amepigwa marufuku kutumia choo cha wenyewe.Baada
ya kupigwa marufuku akarudi kwa baba yake ambae amepanga chumba na
sebule.Baba na mama wanalala chumbani yeye analala sebuleni.
Sebule katika nyumba yake hiyo ambayo ipo Yombo dovya.
Huyu ndio jirani mwenye choo chake lakini amepigwa marufuku
Hapa ni chumbani kwake.
Kama
ambavyo amesikika kwenye leo tena Mwazani anaomba kusaidiwa pesa ili
aweze kujenga choo.Iwapo uliguswa na matatizo yake mchangie kwa namba
0759 789863 na 0657 795654.