Like Us On Facebook

BABA MZAZI WA MWANADADA WEMA SEPETU AFARIKI DUNIA.....

Wema-Sepetu
Siku chache tu baada ya kuanza kurushwa hewani kwa kipindi halisia cha televisheni(Reality Show) yake, muigizaji, mrembo maarufu nchini Tanzania (Miss Tanzania 2006),Wema  A. Sepetu, amepatwa na msiba mkubwa. Amefiwa na Baba yake mzazi,Balozi Isaac Abrahamu Sepetu.
Taarifa ambazo BC imezipata zinapasha kwamba Mzee Sepetu ambaye kwa muda wa miezi kadhaa sasa amekuwa akiugua na kusumbuliwa na maradhi ya kiharusi,. Mzee Sepetu alikuwa pia akisumbuliwa na kisukari.Amefariki jijini Dar-es-salaam. Mipango ya mazishi inafanyikia nyumbani kwa marehemu maeneo ya Sinza-Mori jijini Dar.



Wema2 
Wema katika picha ya pamoja na baba yake mzazi,Balozi Abraham Sepetu. Pembeni ni rafiki wa karibu wa Wema,Petitman

Balozi Sepetu aliwahi kuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje mnamo miaka ya 1970 wakati wa utawala wa awamu ya kwanza chini ya Mwalimu Julius Kambarag Nyerere.  Vilevile, aliwahi kuwa balozi nchini Urusi tangu mwaka 1982 wakati wa utawala huohuo wa Nyerere.
Pia, Machi 27, mwaka huu, Balozi Sepetu aliteuliwa na Rais wa Zanzibar, Dr Mohammed Shein,  kuendelea kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Uwekezaji Vitegauchumi ya Zanzibar (ZIPA).
Mwenyezi Mungu ailaze roho ya Marehemu mahali pema peponi.
TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII
KAMA UMEGUSWA NA HABARI ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.
 

KILELE CHA HABARI Copyright © 2014 -- Template created by Mbatta -- Powered by Kilelechahabari