Jose Chameleone ameibuka mshindi
kwenye tuzo za BEFFTA, tuzo kubwa za Ulaya kwaajili ya watu weusi ambazo
huwatuza watu kwenye burudani, fashion, televisheni na sanaa.
Chameleone alikuwa ametajwa kuwania kipengele cha Best International Act na alikuwa akishindana na wasanii wengine wakiwemo Rihanna na D'Banj.
Tuzo hizo zimetolewa jana Ijumaa na leo Jumamosi pia huko jijini London.
Kupitia Facebook, Chameleone ameandika kuelezea furaha yake baada ya kutwaa tuzo hiyo:
"It's hard to fully express my gratitude towards all of you who appreciate My MUSIC, and love AFRICAN music at large. You are the reason I have managed to add another onto my list and rankings. Am fresh and still jubilating with you This joyous feeling in me i congratulate my fans worldwide, we did this together i have just won BEFFTA AWARDS BEST INTERNATIONAL ACT- DR JOSE CHAMELEONE."