Mara baada ya kuona wenzake wakiwa mikononi mwa nguvu za dola katika kamatakamata ya polisi, mrembo huyo ambaye baadaye alijitambulisha kama mchumba wa mtu, alianguka ghafla na kuzimia kiasi cha kuzua hofu miongoni mwa machangu wenzake walioangua kilio wakidhani mwenzao amekata ringi (kufa).
Baada ya muda msichana huyo alirejewa na fahamu akiwa mikononi mwa polisi na kuanza kuangua kilio akiomba asikamatwe kwa kuwa yeye ni mchumba wa mtu na atakuwa kwenye wakati mgumu kama mchumba’ke atajua anajiuza.
“Naomba msinikamate. Mimi ni mchumba wa mtu afande. Mtaniweka kwenye wakati mgumu kama akijua nilikuwa nikijiuza. Jamani nitamkosa mchumba wangu Luka,” alisema mrembo huyo huku akiomba maji ya kunywa.
Hata hivyo, kilio chake hakikuwazuia ‘OFM’ kufanya kazi yake ndani ya Kituo cha Polis