SIKU moja baada ya Rais Jakaya Kikwete kukasirishwa na kauli ya Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema) Tundu Lissu, kuwa Rais hakuheshimu mapendekezo ya TEC, CCT na walemavu huku akisema kwamba maneno ya Mbunge huyo niya uzushi na uongo mtupu, nanin ya unafiki, fitina na uzandiki wa hali ya juu. Mbunge huyo ameibuka na kumjibu Rais Kikwete.
Nanukuu sehemu fupi ya hotuba ya Rais:
"Siyo tu kauli hiyo ya Mheshimiwa Tundu Lissu ni uzushi na uongo mtupu bali pia ni ya unafiki, fitina na uzandiki wa hali ya juu.
"Nasema hivyo kwa sababu, sipendi kuamini kuwa Mheshimiwa Mbunge amesema yale kwa kutokufahamu ukweli au kwa bahati mbaya.
"Amesema yale kwa makusudi mazima ya kupotosha ukweli ili pengine isaidie kujenga hoja yake ya kutaka Rais asiteue wale Wajumbe 166 wa Bunge Maalum"
Rais Kikwete alisema hayo wakati akihutubia Taifa, kama ilivyo kawaida yake kila mwisho wa mwezi.Katika hotuba yake, JK alisema suala la Mchakato wa mabadiliko ya Katika Mpya haliwezi kuwagawa watanzania kwa sababu katiba siyo mali ya chama.
"Hatutengenezi Katiba ya Chama fulani bali Katiba ya nchi, Katiba ya watu wa vyama vyote na wasiokuwa na vyama ambao ndiyo wengi kuliko wote. Lazima tuongozwe na ukweli huo na tuwe na msimamo huo wakati wote vinginenvyo tutaliingiza taifa kwenye matatizo yasiyokuwa ya lazima", alifafanua Rais Kikwete.
Akizungumza na Gazeti la Tanzania Daiama jana, Lissu ameiponda hotuba ya Rais Kikwete iliyojaa maneno “nimeambiwa” akisema ana uhakika gani wale waliomwambia kama hawakumdanganya?.
“Maneno yaliyotajwa na rais kuhusu uteuzi wa wajumbe toka Shirikisho la Vyama vya Wenye Ulemavu, TEC na CCT yalizungumzwa kwenye kamati sio maneno yangu.
"Kikwete hakuwepo kwenye kamati, mimi nilikuwepo. Sasa mawaziri wake na wabunge wake wa CCM wamwambie ukweli, waache kumdanganya.
“Kikwete amesema mimi ni muongo, mnafiki, lakini hoja ambazo tulizipinga mfano ya ushiriki wa wadau wa Zanzibar, hata Waziri wa Sheria na Katiba wa Zanzibar, Abubakari Khamisi naye ameniunga mkono. Je, na huyu ni mzushi, muongo na mfitini?” . Alisema Tundu Lissu
Aliongeza kuwa hoja ambayo rais anakimbilia kwamba alimzuia asiteue wajumbe 166, ilikuja bungeni mwaka 2011, wakaipinga, ikaondolewa. Lakini mwaka huu wameirejesha tena.
-Habarimpya