Show
 ya TV ‘In my shoes’ ya mwigizaji Wema Sepetu kutoka bongo movie imeanza
 kuonyeshwa Eatv October 16 2013 ambapo Episode hii ya kwanza imeanza 
kwa kumuonyesha Wema kwanza akieleza yeye ni nani, anafanya nini, ni mtu
 wa aina gani na mengine kama hayo ambapo yafuatayo hapa chini ni 
maswali aliyoulizwa na kuyatolea majibu.
Swali: Wema ni nani?
Jibu: Wema Sepetu is a girl, i can say a Lady mwenye umri wa miaka 24 
kutoka familia ya Isack Abraham Sepetu, a darling, a libra.. a girl who 
is very ambicious, i love my self…
Swali: Siku yako ya kwanza shuleni ilikuaje?
Wema: Siku ya kwanza tumeenda nikakutana na msichana flani hivi anaitwa 
Shubira nakumbuka mpaka leo, alikua rafiki yangu wa kwanza tulikutana 
shuleni nilikua na miaka minne… tumekaa nikaanza kulia kwa sababu ilikua
 sehemu mpya, mazingira mapya baada ya hapo tukazoea.
Shule ilikua vipi kipindi unasoma?
Wema: Naweza kusema kipindi ambacho niko shule, Mwalimu wangu sijawahi 
kukaa hata siku moja kumfikiria mara mbili na haijawahi kutokea kwamba 
hata mwalimu akaweza kufanya labda matamanio au kutaka kitu chochote, 
hamna kitu kama hicho
Wema: Ningepata nafasi ya kurudi shule, academic nini uniform na nini… 
ningejaribu kuifanya more fun, a place where everybody can be just 
himself or herself and just be Wema Sepetu kwa sababu right now this is 
my time!!
Swali: Ni nani ambae uko karibu nae kwenye familia yenu?
Wema: Dada yangu wa kwanza kuzaliwa anaitwa Tunu, tunakwenda sawa kwenye
 many many ways, kipindi mama yangu alivyonizaa aliumwa akalazwa hivyo 
dada yangu ndio akawa ananihudumia kama mtoto wake, ananinywesha uji… 
anahakikisha nimekunywa maziwa on time na mpaka leo ananiita my baby and
 I call her my mami… mtu wa pili ni dada yangu wa tatu, she is my 
bestfriend… baba yangu atabaki kuwa baba yangu tu, mama yangu ni my 
gurdian Angel, my heart my darling.

Swali: Ulishawahi kugombana na ndugu zako?
Wema: Yeah nimegombana na dada yangu mpaka sasa hivi hatuongei, sio kitu chepesi….
Swali: Unaamini Mama yako ni mkorofi?
Wema: Linapokuja swala la mama yangu huwezi ukasema kwamba ni mkorofi 
lakini hapendi nikikosea wala kufanya kitu ambacho sicho…. kutokupenda 
kwake inafikia point anakua na hasira sana alafu njia ya kuonyesha 
hasira yake ndio level ya juu, yeye anafikiria kwamba anatengeneza ila 
badala ya kutengeneza ndio anaharibu.

Wema na Mama mzazi
Swali: Wema ni mkorofi?
Wema: Mimi sio mkorofi, mtu ambae hanijui ndio ataniita mkorofi 
ukishanijua yani tutafika mbali lakini usiponijua na hujui ninachonitaka
 ndio tatizo.
Swali: Unajisikiaje kuwa Wema Sepetu?
Wema: Kuwa Wema Sepetu sio kitu rahisi, haiwezi kuwa kama watu 
wanavyofikiria  na haitakua hivyo kwa sababu ni maisha ambayo naishi, ni
 mpaka uone maisha ninayoishi ndio unielewe… yani hata kujaribu kuieleza
 ili uielewe napata tabu… mashabiki wangu wananielewa sana na uhusiano 
wangu na wao ni mzuri na ni tofauti na uhusiano kati yangu na familia 
yangu’

Swali: Unachukulia vipi unaposemwa ama kuandikwa vibaya?
Wema: Katika vitu vyangu ambavyo mtu wa nje anaweza kuviona kama vile… 
Mungu wangu Wema ana nini, mi navichukulia kama changamoto… mi naona 
kuna kitu special kuhusu mimi, kwa nini wasiseme watu wengine?
Swali: Unaamini wewe ni mrembo?
Wema: I am beautiful, naamini kwamba mimi ni beautiful kwa sababu nina pure heart… ni kitu Mwenyezi Mungu alichonibariki nacho.
Swali: Kitu gani unachojivunia kwamba kinakutofautisha na wasanii wengine?
Wema: Ninachojivunia… uelewa wangu, I am very very smart.. ni mtu ambae 
ukiniambia kitu, fasta…. na hata kama sijui kitu, kujiua itanichukua 
muda mfupi, ability kusimama na kuongea na nikasikika, lugha…. hivyo ni 
vitu ambavyo najivunia sana
Swali: Unavuta sigara?
Wema: Ndio, ninapokua na msongo wa mawazo sana huwa nafanya hivyo  ili kuondoa mawazo na inaweza kutokea mara moja kwa mwezi..
Swali: Ni kweli kwamba wewe ni limbukeni wa umaarufu?
Wema: Sijaacha ustaa uniendeshe, unajua kuna wale watu wanaacha ustaa 
uwameze mpaka wanabadilisha kuongea, watu wengine wanaacha ule ustaa 
unawaendesha mwisho wa siku unaanza kuishi maisha ambayo hawana inafika 
point unaishi kama mtumwa mwisho wa siku unaishi maisha ambayo huna, 
unaanza kuumia Mungu wangu nimeshazoea kuishi maisha yale,  ishi vile 
ambavyo unaweza… huna pesa, huna! mimi ni mtu ambae ninaweza kuamka 
nasikia hamu ya kula mihogo, nafanya kitu ninachopenda na sio anachotaka
 mwingine’
Swali: Gucci na Vanny ni kina nani kwako?
Wema: My precious, kipenzi changu ni Vanny, katakufanya tu ukapende…. Gucci staa anajifanyaga kama yeye mtu tu wa kuchil!
Swali: Unaamini katika ushirikina?
Wema: Ushirikina najua kwamba upo, uchawi kama uchawi upo worldwide ila 
sipendi kujishirikisha manake sitaki siku moja kuwa mtumwa, mimi mtoto 
wa Kiislamu nafanya kisomo nachinja kila baada ya muda so naamini 
ukifanya hivyo unajikinga na vitu vingi.

Swali: Umeshawahi kulogwa?
Wema: Nimeshawahi kulogwa, imeshawahi kunitokea kabisa yani… ni kitu kingine ambacho huwa sipendi kukizungumzia.
Swali: Ulishawahi kwenda kwa Mganga?
Wema: Siwezi kuficha, wamekuja wengi ambao wanataka kunipeleka wengine 
mpaka kuniletea Waganga nyumbani kwangu lakini Quran mimi ndio mganga 
wangu namba moja.
Swali: Unafikiri kuna Wasanii wenzako ambao wanakuchukia?
Wema: Unategemea nini once ukishakua katika spotlight, hautegemei kuwa 
na watu wazuri karibu yako lazima wengine watakua ni wabaya na sio kila 
mmoja atakua anakuchekea kwa uzuri, wengine sio kutoka moyoni, 
wanakuchekea tu kwa sababu hawana choice.
Swali: Nani alikua mpenzi wako wa kwanza?
Wema: Sitaki kumtaja bwana….

Swali: Inasemekana unapenda mahusiano ya kimapenzi na watu maarufu?
Wema: Sio kwamba Wema anapenda kuwa na wapenzi maarufu, ni field ambayo 
tuko, tuko kwenye kiwanda kimoja kwa hiyo kwangu imekua iko hivyo, ni 
watu ambao mtakua mna interest zinaendana..
Swali: Umeshawahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na watu wangapi?
Wema: Wanne, watano au Wanaume sita hehhehe!!
Swali: Mlianza vipi mapenzi na Diamond?
Wema: Tulikua na hii Chemistry inaendana ilikua crazy, baada ya yeye 
kuniandikia msg kwenye facebook na kuniambia ananipenda, ni mtu ambae 
nilipata uzoefu mapenzi yanaweza kuwaje, nilipitia kwenye furaha na 
huzuni nikiwa na yeye…. kilichotokea kimetokea
Swali: Kuna ushindani wowote kati yako na Diamond?
Wema: Once upon a time kulikua na Diamond na Wema, na hawa watu walifall
 inlove…. watu wanajaribu sana kutulinganisha au tunaonekana 
tunashindana labda kwa sababu yeye anafanya vizuri kwenye industry yake 
na mimi nafanya vizuri kwenye industry yangu, mi sijawahi hata siku moja
 kushindana na Diamond…. mi kuimba siwezi.

Wema na Kajala Masanja
Swali: Kajala Masanja ni nani kwako?
Wema: Kajala ni rafiki, dada…. ndugu ambae hayuko kwenye ukoo wa Sepetu 
lakini uhusiano wangu na wake kwenye urafiki toka mwanzo sidhani kama 
nimewahi kuwa na uhusiano huu na mtu yeyote, watu wanadhani kwamba 
nimeanza kumjua juzi… tokea mwaka 2007 mi nimeanza kumfahamu Kajala 
mpaka tukawa marafiki sana hadi tunajikuta tumevaa sare.
Swali: Wazo la kumtolea Kajala dhamana ya milioni 13 lilitoka wapi?
Wema: Nilimuangalia Kajala analia pale kizimbani, aidha ilipwe faini au 
aende jela…. kilikua ni kitu ambacho hakijapangwa, ilikua suprise kwetu 
wote ila nilichokua nataka ni Kajala kuwa huru kwa hiyo kilichoweza 
kufanyika kilifanyika.
Swali: Ulijisikiaje siku tatu ulizolala Mahabusu?
Wema: Haikua nzuri kabisa, ni siku tatu mbaya kwenye maisha yangu… 
hakuna binadamu ambae hapendi uhuru, kwanini nilimsaidia Kajala na 
kupata nguvu ya kutoa hizo milioni 13? kwa sababu nimekuepo hapo… mimi 
siku tatu zilikua balaa sasa mwenzangu mwaka mmoja naa? ingekuaje? hata 
kama nisingemsaidia Kajala alafu Kajala ndio angekaa miaka hiyo 7 sijui 8
 jela mimi nisingeweza kuishi, sio Wema Sepetu alivyo’
Swali: Best Werema ni nani katika kampuni yako?
Wema: Bestizzo ni blogger wangu na mpiga picha wangu, anarun kila kitu kinachohusu kampuni kwenye social network Website nini…
Swali: Kwanini uliamua kufanya nae kazi?
Wema: Kipindi cha kwanza niliona kumpa kazi ingeleta matatizo flani 
lakini nikafikiria, namjua Bestizzo alikua akifanya kazi kwa Diamond na 
alikua mfanyakazi mzuri, sijui ni kitu gani kilimfanya aondoke kwa 
Diamond kwa sababu mimi wakati sikua kwenye uhusiano mzuri na Diamond, 
Best bado alikua kwa Diamond na kipindi hicho hata bado nilikua 
sijafungua kampuni, hata alikua haniombi kazi ila alihitaji 
nimuunganishe na wengine’

Tiny Dad na Petit
Swali: Uko vipi na Tinny Dad, Pettman na Martin Kadinda?
Wema: Tiny na Petti ni watu wangu wa karibu sana, nimewajua kwa muda 
mrefu na wananijua na ninawajua.. Kadinda kabla ya kuwa meneja wangu 
alikua rafiki yangu, hakua rafiki yangu wa hivyo… tulikua hatuonani hata
 miezi sita lakini tukikutana namwambia yote yaliyopita, mwaka juzi ndio
 Martin akasema ngoja niwe Meneja wako, hatukua hata na mikataba 
mwanzoni… tukajaribisha na tukafanikiwa mpaka leo niko nae.

Wema na meneja Martin Kadinda
 
 
 


