Like Us On Facebook

MAJUTO: "KWASASA NALIPWA KUANZIA MILIONI 17 MPAKA 20 KWA MWEZI


Ni nadra sana kwa  staa  wa Tanzania kukubali kusema kiwango anachopata kwa mwezi kutokana na kazi yake ya umaarufu ila kwa Mzee Majuto hali imekuwa ni kinyume...

Akiongea  na  Millard Ayo, mzee Majuto amekubali kusema kila kitu kwenye kipato cha movie zake za vichekesho ambazo mpaka sasa ndio zinashika nafasi ya 1 kwa mauzo Tanzania

Akiwa ni baba wa watoto tisa, mzee Majuto  amefunguka  kuwa   kwenye movie za kuigiza sasa hivi kama mtu akitaka kumshirikisha ni lazima amlipe milioni nane kutoka milioni 2 au tatu alizokuwa anazikusanya mwanzoni....

Bei  hiyo  ameibadili kuanzia mwezi September 2013  kwa sababu  kadri anavyocheza movie nyingi za kushirikishwa ndivyo anavyozidi kujipunguzia kipato chake  kwa mwezi kutoka kampuni ya STEPS iliyomwajiri’
 
"Mpaka sasa nimecheza movie zaidi ya 600 toka nimeanza kuigiza  ( za kushirikishwa na zake mwenyewe) ...


"Nilianza kulipwa zaidi ya milioni moja kwenye movie toka mwaka 2007/2008 baada ya kuwa na kampuni ya Ally Riyami ambayo  ilikuwa inanilipa shilingi laki sita kwa kila movie ya Comedy kwa hiyo kwa mwezi nilikuwa napata mpaka  milioni 6 au saba kutokana na idadi ya movie nitakazoigiza’ – Mzee Majuto

"Kwa sasa hapa Steps nalipwa kuanzia milioni 17 mpaka 20 kwa mwezi, ni malipo mazuri sana ambayo napata kila mwezi na nimepangiwa kucheza movie 9 kwa mwaka lakini kule Ally Riyami kwa mwezi ndio nilikua nacheza hizo movie 10, yani unacheza movie mpaka unasikia kizunguzungu…. 

"Nilitakiwa kucheza movie 1 kila baada ya siku tatu ila kwa sasa kwenye mkataba wa Steps nacheza movie moja ya kampuni na moja ya nje ya kampuni, maisha mazuri’ – Mzee Majuto.

Credit-Millardayo
TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII
KAMA UMEGUSWA NA HABARI ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.
 

KILELE CHA HABARI Copyright © 2014 -- Template created by Mbatta -- Powered by Kilelechahabari