Like Us On Facebook

KIOO KILINIFANYA NIFANYE MAPENZI NA SAJUKI..WASTARA

Wastara   amefichua  siri kwamba kioo ndicho kilisababisha aanzishe uhusiano wa mapenzi na marehemu Juma Issa Kilowoko ‘Sajuki’ aliyefariki Januari 2, mwaka huu..
 
Wastara aliweka bayana kuwa marehemu Sajuki ambaye alikuwa mumewe, hakuwahi kumtongoza lakini kioo ndiyo kilikuwa chanzo kilichosababisha wajikute wameingia dhambini kwa mara ya kwanza.
 
Akizungumza na gpl, Wastara alisema kuwa siku hiyo walikuwa wakifanya mazoezi ya filamu moja (hakutaja jina) nyumbani kwake na Sajuki alikuwa muongozaji wa sinema hiyo.
 
“Ilikuwa ni usiku wa manane tukiwa nyumbani kwangu tukifanya mazoezi ya filamu moja, sasa ilikuwa ni scene ya mapenzi tukawa mbele ya kioo huku tumekumbatiana.
 
Tukaendelea hivyoo, mmh! Sasa tulivyokitazama, tukahisi tunaendana. Tukaendelea kujifanyia tathmini na ghafla tukajikuta tunafanya kweli, kioo kilisababisha tukajikuta tunafanya mapenzi,” alisema Wastara kwa uso wa aibu..



-GPL
TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII
KAMA UMEGUSWA NA HABARI ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.
 

KILELE CHA HABARI Copyright © 2014 -- Template created by Mbatta -- Powered by Kilelechahabari