Rais
Kikwete amenukuliwa na RADIO WAPO akisema kuwa kama angekua na Uhuru wa
kutembea bila Ving’ora angefanya ziara za kushtukiza kwa Wakuu wa
Wilaya(DCs) na Wakuu wa Mikoa(RCs) kutokana na kukithiri kwa vitendo vya
uzembe.Amedai
Kauli hii ya Rais imekosa viwango vya Urais na
weledi wa Amiri Jeshi Mkuu wa Ulinzi na Usalama.Ni kauli isiyokua na
umaarufu wala umakini wowote.Kauli hii yenyewe ni Taswira ya uzembe na
kushindwa kwa Taasisi ya Urais.Kwa Nchi zinazojali heshima ya mamamlaka
ya Urais ingebidi Rais ashinikizwe ashinikizwe kujiuzulu
Rais
anakiri kuwa nchi imemshinda,mamlaka ya Urais hayapo kitaasisi
tena.Rais anakiri kuwa Usalama wa Taifa (TISS) hauwezi kufanya kazi hadi
Rais afanye kazi za kuvizia
Tumezoea
kushuhudia mtindo huu wa kuvizia ukifanywa na matrafiki
barabarani,wanajificha vichakani na kujitokeza ghafla magari
yanapokaribia mahali walipojificha.Mtindo huu umeingia Ikulu
Tumegeuka
kuwa taiafa la kuvizia.Hivi Rais atavizia na kushtukiza idara
ngapi?Watu wazima na wasomi hadi wasukumwe?Hakuna working policy?Semina
Elekezi hazikufanya kazi? Je,Majina aliyokiri kuwa nayo ya wauaza madawa
ya Kulevya alishindwa kuchukua hatua kwa sababu ya ving’ora?
Kumbe
Ving’ora ndiyo kikwazo kwa Rais kuwacukulia hatua wezi wa EPA? Siku
hizi Matamshi ya mkuu wa Nchi yanazidi kutia mashaka sana.Kauli zake ni
tata.
Leo
amevilaumu Ving’ora kwamba vinamzuia kufanya ziara za kufamania.Haamini
tena katika mfumo imara wa kiutendaji bali weledi wa kufanya
fumanizi.Ndiyo Tunajenga taifa kubwa namna hii?
RADIO WAPO...
TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII
KAMA UMEGUSWA NA HABARI ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.