Na Frank Geofray-Jeshi la Polisi. 
Aliyewahi kuwa Kamanda wa Polisi Kikosi cha usalama barabarani, Kamishna Msaidizi Mwandamizi (SACP) mstaafu James Kombe amefariki dunia wakati akipatiwa matibabu katika hospitali ya Ocean Road jijini Dar es Salaam.

Akizungumzia
 kifo hicho Msemaji wa Jeshi la Polisi Nchini, Mrakibu Mwandamizi wa 
Polisi (SSP) Advera Senso alisema, Kombe alifariki Oktoba 22 mwaka huu 
na taratibu za mazishi zinaendelea.
Aidha
 Senso alisema Marehemu Kombe alizaliwa mwaka 1950 huko Mwika mkoani 
Kilimanjaro na alijiunga na Jeshi la Polisi tarehe 15 mwezi machi mwaka 
1970 baada ya kuhitimu elimu ya sekondari mwaka 1969 nchini Uganda 
ambapo alipandishwa vyeo na kupewa madaraka mbalimbali.
Baadhi
 ya nafasi alizowahi kuzitumikia katika Jeshi la Polisi ni pamoja na 
kuwa Mkuu wa Polisi wa Wilaya (OCD) katika wilaya za Dodoma, Tarime, 
Serengeti na Arusha pamoja na Kuwa Mkuu wa Polisi wa Mkoa (RPC) katika 
mikoa ya Lindi, Arusha, Kigoma pamoja na Mkuu wa Kikosi cha Kutuliza 
ghasia Tanzania na hadi anastaafu alikuwa mkuu wa kikosi cha Usalama 
barabarani Tanzania.