Kulwa Kikumba ‘Dude’. |
STAA wa filamu Bongo, Kulwa Kikumba ‘Dude’ ameshushiwa madai mazito kuwa ameingia penzini na kimada wa mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (jina tunalo), aliyetajwa kwa jina maarufu la Fetty. Kwa mujibu wa chanzo makini ambacho kiko karibu na msanii huyo, mbunge huyo kwa sasa ameshagundua kuwa Dude ana uhusiano na ‘nyumba ndogo yake’ hiyo. Taarifa hizo zilizidi kudai kuwa, hapo awali mheshimiwa huyo ‘hakukausha nyayo’ kwa mrembo huyo lakini baada ya kugundua hali ya ‘sintofahamu’ baina ya Fetty na Dude, amesitisha ukaribu na mrembo huyo. Baada ya kutonywa habari hizo, paparazi wetu alimtafuta Dude ili kujua ukweli wa mambo, alipopatikana alisema:
“Ni kweli hata mimi hizo habari nimezisikia kutoka kwa wasanii wenzangu na zinaniumiza sana kwani mimi najua Fetty ana bwana wake tena mheshimiwa. Naogopa sana kutekwa, naomba kupitia gazeti hili huyo mheshimiwa aelewe kwamba mimi sina uhusiano mbaya na mwanamke wake, tumefahamiana kupitia filamu tu,” alisema Dude. Fetty alipotafutwa kwa njia ya simu, iliita kwa muda mrefu bila kupokelewa.