Vitendo vya madirector wengi wa filamu kupenda kuwarubuni wasanii wachanga kuwa kama watatoa uroda basi watapewa nafasi ya kucheza filamu na kuwa mastaa wakubwa imemtokea puania msanii na director maarufu wa bongo movie Edward Nicas Temu maarufu kwa jina la Nicas baada ya kufumaniwa na mke wa mtu ambae ni msanii wa kundi lake.
Jina la Nicas ni jina maarufa sana hasa kwa wasanii kufutia huyu mshikaji kuwa kwenye sanaa kitambo akiwa kama msanii na director .Kwa kipindi kirefu amekuwa akifanya kazi za watu lakini siku za hivi karibuni alianzisha kundi lake huko maeneo ya Kinondoni Moscow na kukusanya makumi ya wasichana kwa ajili ya kucheza filamu zake...
Kutokana na wakidada wengi hasa Underground kupenda kuigiza, jamaa huyo alijikusanyia warembo wa kila aina na alifanikiwa kuwachezesha filamu zake tatu Bad Father,The Reason,House Girl N Boss...
Habari zaidi zinaripoti kuwa baada ya kumaliza kuwachezesha filamu hizo msanii huyo alianza kumuweka karibu mmoja wa wasanii wake ambae ni mke wa mtu anayeishi na mumewe maeneo ya Kawe Jijini Dar.
Akiongea na Xdeejayz , mume wa mischana huyo Abdula Sanga alilaani kitendo cha boss wake kujimegea mkewe kwa kofia ya cheo chake.
" Nampenda sana mke wangu na ndio maana nilikuwa nimemruhusu akafanye sanaa lakini baadae niliambiwa na shoga yake kuwa kuwa bosi wake anataka kumla uroda ili amuweke kwenye kava ya cd ya filamu yake na kama hatotoa uroda basi hatamuweka" Alisema kijana huyo ambae ni mfanyabishara.
Abdula Sanga aliendelea kusema baada ya hapo alimuomba huyo rafiki na mkewe ampe ushirikiano ikiwa ni pamoja na kumuhabarisha hatua kwa hatua ambapo hadi siku ya tukio alitaarifiwa ni wapi wanapokwenda kupeana uroda...
"Niliandaa askari wangu na tukaweka mtego Guest iitwayo Bundo iliyopo Kinondoni Moscow na hatimae mtego wangu ulinasa na kumfuania mke wangu live akiwa na huyo bosi wake wa sanaa" Alisema Sanga kwa jazba.
Mwandishi wetu alishuhudia kindomu tano zilizotumika ndani ya chumba hicho .Kwa tafsri ya haraka haraka ni kwamba tayari mke huyo alikuwa ameshaliwa mara tano, hali iliyoamsha hasira za mume wa mke huyo na kuanza kumvurumushia makonde msanii huyo hadi polisi walipoingilia kati.
Picha zaidi za tukio hilo:
<<PICHA YA KWANZA>>
<<PICHA YA PILI>>
<<PICHA YA TATU>>
<<PICHA YA NNE>>
<<PICHA YA TANO>>
<<PICHA YA SITA>>
Source-Xdeejayz