MWANADADA anayefanya vizuri kwenye tasnia ya filamu za Kibongo, Jacqueline Wolper Massawe ‘Gambe’ ameamua kudumisha mila na desturi baada ya kupiga picha akiwa anakunywa pombe ya kienyeji aina ya mbege.
Wolper alitundika picha hiyo katika mtandao wa Kijamii wa Instagram akiwa ameshikilia kikombe maarufu kinachotumiwa na watu wa Kilimanjaro kwa ajili ya kunywea pombe aina hiyo na kuambatanisha na maneno kuwa anadumisha mila.
“Nyumbani Arusha nikinywa wine nitakosea jamani, leo mbege tu Wachaga mtanielewa tu,”aliandika Wolper.
Baada ya kuweka picha na maneno hayo watu mbalimbali walionekana kumfagilia staa huyo na kumsifu kwamba ameonesha kujali mila tofauti na watu wengine pindi wanapokuwa mastaa huzibeza mila zao.
Mashabiki wengi walikuwa wakimpongeza kwa kumuandikia maneno kwa lugha ya Kichaga kuonesha kwamba wamemkubali.