Like Us On Facebook

UKICHECHE NDO ULIOSABABISHA REAL MADRID KUMUUZA OZIL

                  MCHEZAJI mpya wa Arsenal aliyesajiliwa kwa dau la rekodi, Mesut Ozil ametuhimiwa kujichosha mwenyewe kwa kulala na walimbwende sababu iliyofanya vigogo wa Hispania, Real Madrid waamue kumuuza.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24, aliyehamia Arsenal kwa Pauni Milioni 42.5 katika siku ya mwisho ya usajili, aliambiwa na Real Madrid kuweka kazi yake ya soka mbele baada ya kuonekana kuelemewa na penzi la aliyekuwa Miss Venezuela, Aida Yespica, kwa mujibu wa gazeti la El Mundo la Hispania.
Big-money: Ozil completed his £42.5million move to the Emirates on deadline day
Mkwanja mnene: Ozil ametua Arsenal kwa Pauni Milioni 42.5
Venezuelan showgirl Aida Yespica
Aida Yespica

Amemshika: Ozil anafikiriwa kutekwa kimapenzi na aliyekuwa Miss Venezuela, Aida Yespica ambaye amekuwa akimfuata poppote Ulaya anapokwenda kucheza

Ozil ameripotiwa kusafiri hadi Italia kila anapopata mwanya kidogo ili kupata fursa ya kuwa na mwanamitindo huyo mwenye umri wa miaka 31 mjini Milan au katika hoteli yake mjini Paris.
Anakadiriwa kutumia kiasi cha Pauni 15,000 kila wiki mbili kwa ndege binafsi, inayompeleka kwa Yespica.
El Mundo limeripoti kwamba safari za asubuhi na mapema zimezidi na kiasi cha kufikia kushusha kiwango chake cha soka.
Controversial: Some Madrid fans and players are dismayed by the sale of Ozil
Utata: Baadhi ya mashabiki wa Madrid wamekasirika juu ya kuuzwa kwa Ozil
Mpenzi wake mpya, Many Capristo anafikiriwa kutaka kumfuata Uingereza ili kuwa karibu naye, lakini gazeti la The Sun le leo limeripoti kwamba amekaa ushauri wa kutafuta nyumba karibu na viwanja vya mazoezi vya Hertfordshire.
Capristo anayetarajiwa kuwa nyota mpya katika wake na wapenzi wa wachezaji, maarufu kama WAGs - mahusiano yake na mwanasoka huyo yamepewa jina Posh na Becks wa Ujerumani.
Ozil, mwenye asili ya Uturuki, ni Muislamu, lakini mpenzi wake amekuwa maarufu Ujerumani kwa sababu ya muziki na kudansi katika show ya Televisheni
Mesut Ozil
Mandy Capristo

Penzi la nguvu: Mesut Özil na mpenzi wake mwimbaji, Mandy Capristo wanatarajiwa kuhamia London baada ya mchezaji huyo kujiunga na Arsenal akitokea Real Madrid kwa Pauni Milioni 42.5
Together: The couple have been dating for less than a year but seem particularly loved-up
Pamoja: Wawili hao wamekuwa kwenye wimbi la mahaba kwa zaidi ya mwaka.
-BIN ZUBEIRY
TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII
KAMA UMEGUSWA NA HABARI ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.
 

KILELE CHA HABARI Copyright © 2014 -- Template created by Mbatta -- Powered by Kilelechahabari