AKIWA amepoteza heshima yake ya mwanasoka ghali duniani kwa Gareth Bale, wazi Cristiano Ronaldo atapenda kumuonyesha mchezaji mwenzake huyo mpya Real Madrid nani ni babu kubwa Bernabeu.
Katika siku ya tatu tu ya mazoezi yake kamili klabu hiyo mpya, Bale tangu ajiunge nayo kutoka Tottenham kwa Pauni Milioni 86, alijikuta akipitiwa kwanja na nyota huyo wa zamani wa Manchester United ambaye bila shaka alitaka kumuonyesha 'mchawi huyo wa Wales' kwamba si kazi rahisi kuwa mkali Real.
Pia Pepe alionekana kuchekelea wakati akiangalia Mreno mwenzake, Ronaldo akimtenda kitu Bale kwa kumrukia kwenye kifundo cha mguu.

Cheki kitu hicho: Cristiano Ronaldo akimpitia miguuni Gareth Bale

Anamfuata: Ronaldo akimrukia Bale

Mguu umefika: Ronaldo akipeleka mguu wake kupitia mpira miguuni mwa Bale

Maumivu: Bale akipewa kitu na Ronaldo
Bale alionekana kuwa sawa tu baada ya kitendo hicho, lakini hakuonekana kuwa mwenye furaha baada ya hapo.
Ronaldo alikuwa anashikilia rekodi ya mchezaji ghali wa dunia wa awali kwa Pauni 80 alizonunuliwa kutoka Manchester United mwaka 2009 na kwa picha hizi inaweza kuchukuliwa kama ni wivu wake kwa mchezaji mwenzake mpya Bernabeu.

Zizou alishuhudia: Ronaldo na Bale wakigombea mpira huku kocha Msaidizi, Zinedine Zidane (kulia) akiangalia

Bale na Ronaldo

Ronaldo akimuonyesha Bale

Ronaldo alianza kwa mazungumzo na Bale


Ronaldo akifurahia na Bale na kumpa dole

Ronaldo akicheza na mchezaji mwenzake zamani Bale Spurs, Luka Modric

Ronaldo akitaniana na Modric pembeni ya Bale