Hali ya
wanawake inazidi kuwa mbaya ndani ya nchi yao TANZANIA inayosifiwa kuwa ni
Kisiwa cha Amani (Amani kwa wanaume) Tukio hili lilitokea mapema mwezi wa nane
mwaka huu Kijiji cha Nyantira Tarime Mara. Katika mazungumzo yake huyu binti
alisema kwamba anatamani sana kurudi nyumbani kwa wazazi wake, tatizo ni kwamba
kwa kuwa alilipiwa MAHARI na mume wake (aliyemkata panga mguu na kuutoa) hawezi
kurudi kwao , wala mama yake hawezi kumkubalia arudi kwao ni mpaka baba yake
aje atoe ruhusa ya yeye kurudi nyumbani au abaki kwa mume muuaji avumilie-MFUMO
DUME UMEKAMATA MIZIZI (mbayaaaaa, sanaaaa. anajisemeaga Mch Rwakatare)
Samahani
kwa picha mbaya, lakini hatuna budi kuonyesha unyama uliopita kipimo ambao
wanawake wanaupitia. Na huu ni mfano halisi kwa mwanamke huyu wa Tarime Musoma.
picha ya juu ni kipande cha mguu wa huyo binti ambao mume alipitisha panga
mithili anakata muwa, picha inaonyesha mguu uliobaki na mguu wa kushoto pia
ulikatwa lakini haukutoka, pamoja na mkono wake wa kushoto ulikatwa lakini
haukutoka. ( Kumbuka tupo kwenye maandalizi mazito ya kuandimisha siku 16 za
kupinga ukatili dhili ya Wanawake)
Mama
mzazi wa binti aliyekatwa mguu na mkwe wake akilia kwa uchungu mkubwa alipokuwa
anaelezea kisa kilichomkumba binti yake. Ni huzuni kubwa sana ukivaa viatu vya
familia hii. Mama anasema kwa utamaduni wao baba wa mtoto aliyekatwa yaani mume
wake ndiye mwenye dhamana ya kuamua mtoto arudi nyumbani au aendelee kubaki kwa
mume fedhuli aliyemgeuza mwenzake ni pingili la muwa au kitoweo Bucher.
Juu ni
mama na chini ni binti akiwa na mawazo juu ya kupoteza mguu wake kwa sababu tu
mume kaamua kuukata. Huyu binti ameathirika sana kisaikolojia kutokana na
tatizo hilo la kukatwa mguu wake na mume wake. hivyo anaomba asaidiwe arudi
nyumbani kwa wazazi wake, au popote pa kuishi ilimradi aondolewe kwenye
mazingira yale aliyopatia mkasa huo. Mbaya zaidi baba mkwe wake anamwambia
"wewe unaona raha kulala kitandani wakati mtoto wangu analala chini jela)
kwa kauli hiyo huyu binti yupo hatarini zaidi. wanaweza kumuua wapoteze
ushaidi. hata hivyo binti aligusia sababu ya kufanyiwa unyama huo ni mwanaume
kuwa na mwanamke mwingine na kwamba alishahamishia mapenzi huko, na kumuona
yeye kama dudu mtu. (Wakati tunaendelea na maadhalizi ya siku 16 za kupinga
ukatili dhidi ya Wanawake, bado hali ni tete)
Hawa
ndio Washika dau wetu wakubwa serikalini. wanasimamia Wizara ya Jinsia
Maendeleo ya Jamii na Watoto. jamani waheshimiwa sana mko wapi? huku wanawake
twafaaa, mnatusaidia vipi? viti vya bunge vinakalika vipi kwa hali hii? ni lini
wanawake tutapaza sauti zetu ili dunia ijue unyama huu unaoendelea dhidi ya wanawake
wa Tanzania? Wanawake Hatuna AMANI kabisa ndani ya nchi yetu. Wizara na Taasis
mbalimbali, Wadau wa kutokomeza ukatili dhidi ya Wanawake, kuna jinsi ya
kumsaidia huyu mama kwa kumuondoa pale kwenye ile nyumba alimofanyiwa UNYAMA
huu na akapewa makao salama? Usikose kufuatilia Joyce Kiria Wanawakelive EATV
na hapa kwenye ukurasa wetu, ili upate mkasa huu wakati tunajipanga kuendelea
na mapambano ya Ukatili wa Kijinsia dhidi ya Wanawake.
-credit
wanawake live tv