Mambo mengi yameendelea kujitokeza katika tukio la mashambulizi ya Westgate mall jijini Nairobi, Kenya. Kwa mujibu wa Ghafla ya Kenya, mhariri wa gazeti la Sunday Nation amejikuta akipoteza ajira yake baada ya kuweka picha ya majeruhi wa tukio hilo katika ukurasa wa mbele wa gazeti hilo, inayomuonesha akiwa katika maumivu makali.
Mhariri wa gazeti la Sunday Nation la Kenya Eric Obino amepoteza kazi baada ya kuweka picha hiyo katika gazeti la Jumapili iliyopita (Sepember 22).
Pia mwandishi wa kujitegemea Robert Alai ambaye amekuwa mstari wa mbele kutoa updates za kinachoendelea katika tukio la Westgate amethibitisha juu ya kufukuzwa kazi kwa mhariri huyo.
“CONFIRMED: Sunday Nation boss Eric Obino sacked and all his security access at Nation Centre revoked. #WestgateAttack” Alitweet Alai.