Like Us On Facebook

NEYMAR, MESSI WAFUNGA WOTE BARCA IKIUA 4-1 LA LIGA

          WACHEZAJI nyota duniani, Neymar na Lionel Messi wote walifunga mabao jana kwa mara ya kwanza wakati Barcelona inaendeleza wimbi lake la ushindi La Liga kufuatia ushindi wa 4-1 dhidi ya Real Sociedad Uwanja wa Nou Camp.
Barcelona imeendeleza rekodi nzuri katika harakati za kutetea taji, huku Neymar akifunga bao lake la kwanza La Liga na Messi akifunga bao lake la saba msimu huu.
Neymar alifungua karamu ya mabao ya Barca dakika ya tano, kabla ya Messi kufunga la pili dakika tatu baadaye, Busquets la tatu dakika ya 23 na Bartra kuhitimisha dakika ya 77.
Bao pekee la kufutia machozi la wageni lilifungwa na De la Bella dakika ya 64.
Kikosi cha Barcelona jana kilikuwa: Valdes; Alves, Pique, Mascherano, Adriano; Busquets, Xavi, Iniesta; Sanchez, Messi na Neymar.
Real SociedadBravo; Estrada, Cadamuro, Martinez, De la Bella; Bergara, Ros, Prieto, Sangalli; Seferovic, Griezmann.
Lionel Messi
Wawili, mawili: Lionel Messi akishangilia bao lake alilotengenezewa nafasi ya kufunga na Mbrazil, Neymar 
Neymar
La kwanza kati ya mengi: Neymar akipiga ngumi hewani kushangilia bao lake la kwanzkufunga La Liga
Neymar
Kijana kutoka Brazil: Neymar akipongezwa na wachezaji wenzake 
BARCELONA
Neymar
Hisi upendo: Neymar na Messi wakionyesha watoto wao kabla ya mechi na kulia wakipongezana baada ya mechi
Sergio Busquets
Mtu mrefu: Sergio Busquets (katikat) akiwapa tano wenzake baada ya kufunga
 Lionel Messi
Mashine: Lionel Messi akijaribu kupasua ukuta wa Sociedad 
Marc Bartra
Bao la mwisho: Beki wa Barca, Marc Bartra (wa pili kushoto) alihitimisha karamu ya mabao ya Barca kwa bao la nne
Barcelona
Mchuano: Sergio Busquets (kushoto) akigombea mpira na mshambuliaji wa Real Sociedad, Imanol Agirretxe
Barcelona
Kazi kazi: Andres Iniesta (kulia) akipambana na Inigo Martinez Berridi
Barcelona
Gerard Pique (kushoto) akimtoka kiungo wa Sociedad, Markel Bergara Larranaga 
Alexis Sanchez
Alexis Sanchez wa Barca akigombea mpira na Alberto de la Bella
TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII
KAMA UMEGUSWA NA HABARI ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.
 

KILELE CHA HABARI Copyright © 2014 -- Template created by Mbatta -- Powered by Kilelechahabari