Like Us On Facebook

HATARII:MUME AMRUHUSU MKE WAKE AUZE MWILI ILI WAPATE PESA YA CHAKULA

                   KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida, hivi karibuni mwanamke mmoja aliyejitambulisha kwa jina moja la Aisha (26), mkazi wa Tabata, Dar es Salaam alinaswa akifanya ukahaba na kudai kwamba ana ruhusa kutoka kwa mumewe ambaye hakumtaja jina, Ijumaa lina habari nzito.
           Aisha (26) akiwa kazini kwa madai kuwa karuhusiwa ya mumewe.
Tukio hilo la aibu lilitokea Afrika Sana, Sinza jijini Dar ambako Aisha alisema ndiko anakofanyia biashara yake hiyo licha ya kuishi na mumewe mbali.
AKUTWA CHOBINGO NA KIDUME
Mwanamke huyo ambaye hakuweka wazi kama ana watoto au la, alisema hayo kufuatia kuzuka kwa varangati la nguvu baada ya OFM kumkuta yeye na mwanaume kwenye jumba moja bovu lililopo mbele kidogo ya Kituo cha Afya cha Kijitonyama, jijini Dar.
Baada ya kumulikwa na mwanga wa kamera na kubaini wameingiliwa na mapaparazi, ndipo mwanamke huyo alikurupuka kwa hamaki na kusema:
“Pigeni hizo picha mnadhani nani ana wasiwasi. Kwa taarifa yenu mimi nina mume na mume wangu ndiye aliyeniruhusu nijiuze ili tupate pesa ya kula.


Aisha akiwapiga 'biti' wana OFM.
“Sasa nyinyi kama mnadhani mume wangu akiona picha zangu ataniacha mmenoa. Mume wangu yeye anajua niko wapi saa hizi, hata nikichelewa kuja huku usiku yeye ndiye hunihimiza ili nije kupata pesa.”
Mwanamke huyo aliyatoa maelezo hayo kwa ujasiri mkubwa na bila kujali kwamba anapigwa picha huku akiwa ameshikilia upande wa khanga.
Baadhi ya majirani waliposikia mkwara wa mwanamke huyo walitoka kushuhudia lakini walipokutana na mwanga mkali wa kamera za mapaparazi wetu walirudi majumbani mwao na kujifungia milango huku wakidai hayawahusu na kutoa pongezi kwa OFM kwa kuamua kusafisha eneo hilo sugu kwa ukahaba. 

ILIKUWA OPARESHENI FICHUA MAOVU
Awali, Oparesheni Fichua Maovu ‘OFM’ ilikuwa ikipita katika zoezi lake la kuwafumua machangudoa wa maeneo mbalimbali wilayani Kinondoni, jijini Dar.

...Aisha akizidi kuwakoromea OFM.
Katika zoezi hilo, OFM ilifika Sinza Afrika Sana na kupiga kambi kwa muda huku makahaba wakionekana kuzurura eneo hilo, hasa pembeni ya eneo maarufu la kujidai, Corner Bar.
Makahaba hao walikuwa wamevaa nusu utupu wote, hasa sketi aina ya vimini na vitopu vya mikono mifupi.

WAELEZA KISA CHA KUPENDA KUVAA VIMINI
OFM iliingia kazini kwa kuwauliza ni kwa nini wanapenda kuvaa vimini badala ya suruali ambapo walisema baadhi ya wanaume wamekuwa wakikimbia na suruali zao baada ya kuwapa uroda ndiyo maana wameamua kuvaa vimini kwa sababu wakati wa ngono hawahitaji kuvua nguo yote.
“Zamani tulipenda sana kuvaa suruali maana huwa zinatukaa vizuri na wanaume wanavutiwa, lakini baadhi ya wateja si waaminifu.
“Wengi walikuwa wakitutenda, unakwenda na mwanaume sehemu kwa ajili ya kumpa uroda, cha ajabu akishamaliza, wanakimbia na suruali zetu.
“Sasa vimini vinasaidia, ukifika kwenye eneo la tukio hakuna haja ya kukivua, unakipandisha kwa juu tofauti na suruali lazima uivue yote,” alisema Jack, mkazi wa Kimara, Dar.

USALAMA WAO UPO  KWA BABU
Makahaba hao waliendelea kudai kuwa, kutokana na baadhi ya wateja kutokuwa waaminifu wameamua kujilinda wenyewe ambapo sasa mwanaume anayewataka kimapenzi, baada ya maelewano wanampeleka jirani na eneo wanalotega mingo ambako kuna mlinzi ‘Babu’.
“Siku hizi wanaume si wale wa zamani, wapo wanaotufuata kwa nia ya kutupora, wengine mnakubaliana lakini baada ya kumpa penzi anakimbia au anakupiga kwanza.
“Tulichoamua ni kwamba, mwanaume akitutaka tunampeleka kwa Babu (eneo lenye mlinzi jirani), maana kule akileta fujo au akitaka kukimbia anakumbana na upinzani mkali,” alisema Sina, mkazi wa Mbezi ya Afrikana, jijini Dar.

AFRIKA SANA IMESHINDIKANA?!
Katika opareshani ya siku hiyo, eneo lililoonekana kukubuhu kwa biashara ya ukahaba jijini Dar ni Afrika Sana ambapo ‘wauza sukari tamu’ hao wapo kwa wingi wakitokea maeneo mbalimbali ya jiji.

-GPL
TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII
KAMA UMEGUSWA NA HABARI ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.
 

KILELE CHA HABARI Copyright © 2014 -- Template created by Mbatta -- Powered by Kilelechahabari