Like Us On Facebook

MAFUFU: "NILIBADILI DINI NIPEWE MKE...."


MIEZI kadhaa imekatika tangu msanii wa filamu za Kibongo, Jimmy Mafufu afunge ndoa ya Kiislamu lakini cha kushangaza ameibuka na kusema hakubadilisha dini isipokuwa aliigiza ili apewe mke.Jimmy aliweka bayana juu ya ishu hiyo hivi karibuni alipokuwa kwenye msiba wa muasisi mkuu wa makanisa ya EAGT, Moses Kulola ambapo alisisitiza kuwa kamwe hawezi kubadilisha dini kwani amezaliwa na kukulia katika familia ya kilokole na aliyekuwa akimlea ni marehemu kiongozi huyo.
“Babu yangu mzaa mama ambaye ndiye ameachwa mrithi wa Kulola na alikuwa pia msaidizi wake, Askofu Mwaisabila walikuwa marafiki sana na muda mwingi nilikuwa nikikaa nyumbani kwa Kulola hivyo nimedumu katika misingi ya Kilokole,” alisema Jimmy huku akisisitiza kuwa hata filamu nyingi anazocheza zina maudhui ya dini.


TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII
KAMA UMEGUSWA NA HABARI ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.
 

KILELE CHA HABARI Copyright © 2014 -- Template created by Mbatta -- Powered by Kilelechahabari