Kilichomponza Masogange kukamwatwa ni pale alipochelewa kutoka uwanjani hapo kutokana na kujiremba, kitu ambacho kilisababisha kufanyiwa upekuzi wa dharura na askari ambaye hakujua kuhusu mpango huo.
Taarifa zinabainisha kwamba, baada ya Masogange na wenzake kufanikiwa kupita katika maeneo ya ukaguzi ya uwanja wa ndege wa Oliver Tambo nchini Afrika Kusini, mwenzake waliyesafiri pamoja aliyetajwa kwa jina la Mangunga alifanikiwa kuondoka uwanjani hapo na mabegi matatu yenye jumla ya kilo 60 za madawa hayo ya kulevya bila kujulikana.
"Kilichomponza Masogange ni pale alivyokuwa anajiremba baada ya kuruhusiwa kupita katika vizuizi vyote. Kiuhakika hakukamatwa katika mashine, bali ulikuwa ni ukaguzi usio rasmi uliofanywa na Polisi. Nadhani huyu Askari aliyewashika hakujua kuhusu mpango huo." kilisema chanzo kimoja ndani ya jeshi la Polisi kama ilivyonukuliwa katika gazeti la Tanzania Daima la Tarehe 17/8/2013