Haya ndiyo maneno ya Ray C mwenyewe ambayo yana ujumbe mzuri ndani yake:
Wote hawa tuliokaa hapa(picha hapo juu) tuliathirika na dawa za kulevya na tumepona kwa kunywa dawa moja tu inayoitwa Methadone. Inapatikana Muhimbili na Mwananyamala pekee na ni bure kabisa.
Tunamshukuru sana Mh Jakaya Mrisho Kikwete kwa kutuletea dawa hii.Ningependa kuwashauri walioathirika wa dawa za kulevya iwe wewe,ndugu yako,rafiki,kaka,dada,mjomba,jirani au yoyote aliye karibu na wewe.Usiogope amua tu kwamba unataka kupona na nenda kanywe hii dawa utapona kabisa.”