Moja ya picha zilizomtokea puani Mrembo wa Facebook akiwa na mwanamuziki/msanii Manaiki Sanga walizopiga visiwani Zanzibar msimu wa sikuu ya Idd
Fathiya Alfan "Mrembo wa Facebook" akiwa hoi baada ya kipigo cha mbwa mwizi alichokipata toka kwa mumewe
Mrembo wa Facebook Miss UtaliiDuh nakozi zinauma kumbe? Sitaki tena umaarufu kudadeki!
"Money is Paper" Mrembo wa Facebook na Manaiki Sanga wakila bata za kufa mtu visiwani Zanzibar hii ni moja ya picha zilizomkera mumewe hadi kufikia hatua ya
Zile picha za aibu zilizoongoza vichwa kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii nchini pamoja na nje ya nchi hasa nchini Kenya zilizokuwa zikimuonesha mwanamuziki na msanii wa bongo muvi Manaiki Sanga akiwa na mabint mbalimbali wakiwa kwenye picha utupu sasa tukio hilo limechukuwa sura mpya baada mrembo aliyekuwa mshiriki Miss Utalii 2013 Fathiya Alfani kupigwa nusu ya kupoteza uhai wake na mchumbaake kwa madai ya kumdhalilisha.
Habari za uhakika toka kwa rafiki wa karibu na mrembo huyo ambae amevujisha picha hizi za kupigwa kwa Fathiya aliieleza mtandao huu “ Jamani tumuone huruma Mrembo wa Facebook kwani hali yake sio mbaya amepigwa sana kiasi cha kutolewa nafsi na mchumbaake anaeishi nae huko Buza” Kilisema chanzo hicho
Aidha katika tukio hilo ambalo mtuhumiwa namba moja na Manaiki Sanga aliyeshiriki kwenye filamu za Tikisa, Love Position, Unpassble, Last Coin na Sory my Soni ambayo amecheza kama staa na pia msanii huyo kwenye nyimbo anazotambanazo ni Nafanya Mambo, Ai Wewe Ft Dogo Janja, Twende Sawa Ft prodyuza Mswaki na nyinginezo. Inadaiwa Manaiki kwa sasa anaishi kama digidigi kwa kuhofia kutiwa mikononi na Jamhuri kwa tukio alilolifanya la udhalilishaji wanawake