Akizungumza na paparazi wetu hivi karibuni, Chaz Baba alisema anamshukuru Mungu kwa kuwa mkewe, Rehema Sospeter ni muelewa hivyo atakapokuwa mzigoni usiku, hawezi kuwa na hofu.
“Mimi na mke wangu tumedumu kwenye uchumba kwa takriban miaka minne hivyo ananijua kiundani na mimi namjua pia, hatuwezi kutofautiana,” alisema Chaz. Mkali huyo alitarajiwa kurudi jukwaani Ijumaa hii (jana) baada ya kumalizika kwa fungate lake