LICHA ya kuonekana sharobaro, msanii mwenye makeke mengi awapo stejini, Ali Salehe Kiba juzikati alinaswa na kamera zetu akipika vitumbua huku akionekana mwenye uzoefu katika mapishi hayo.
Mpango mzima ulikuwa nyumbani kwao maeneo ya Kariakoo jijini Dar ambapo jamaa huyo alibambwa akiwa katika mishemishe za kuandaa vitafunio hivyo ambavyo vilikuwa sehemu ya futari waliyoiandaa yeye na familia yake kwa ajili ya kuwafuturisha watu.
Kitendo hicho kiliwafurahisha mashabiki wake ambapo baadhi yao walisikika wakisema kuwa, msanii huyo ni mfano wa kuigwa kwani ni staa mkubwa sana lakini anapenda kujichanganya na kutosahau asili yake.