Like Us On Facebook

KITANDANI ZAIDI:NYAMA YA ULIMI MPE LAAZIZI WAKO BHANA...SOMA ZAIDI HAPA

MMMH mshaanza eti nimeisha ingia mama Chaunabe kitanga na njia nisiye na bleki kwenye domo langu, wahenga wanasema kinywa cha mkubwa kinanuka lakini maneno hayanuki. Najua maneno yangu ya shombo huenda hayakufurahishi wewe ambaye kila kukicha unabadili wanaume na kuonekana una hila.

Shutuuu dada mwanamke tabia babu wee, mwanamke kujua mumeo anataka nini, mwanamke kujituma kwenye kiwanja kifupi cha sita kwa sita.

Unasahau cha kumvutia mwanaume unakimbilia kuukoboa mwili nani kakuambia weupe mali? Basi mkaa usinge nununuliwa!
Tena leo nakazi na wewe, nani kakuambia weusi ni laana. Basi leo nataka nikuambie wewe usiye na haya uliyemaliza vipodozi mwisho wa siku uso unakuparama kama mchawi mzee, unalo hilo?

Siri ya weusi maana yake ni utamu hata zambarau tamu ni nyeusi, zabibu tamu ni nyeusi na hata usingizi mtamu unapatikana usiku mweusi. Huoni Mzungu akimuonja mswahili anachanganyikiwa.
Wewe unajikoboa Mzungu ajipake masizi? Acha ubwege.

Nimejikuta hata nikisahau kuelezea nilichokikusudia kwa ajili ya malimbukeni wachache, jivunie weusi wako babu wewe.

Tuachane na hayo ambayo kwa kiasi nimejikuta nikipandwa na mzuka na kuingia kwenye mada nyingine. Kama unabisha mwangalie jirani yako anayetumia mkorogo ngozi kama kuku wa mayai aliyezeeka badala ya kupendeza anabakia kituko mtaani.

Acha niendelee na kilicho nitoa nyumbani, shoga leo nilitaka kukuelezea kitu kimoja kuhusinana na tabia  za baadhi ya wanawake kukosa lugha tamu ndani ya nyumba zao kushindwa kuwalisha waume zao nyama ya ulimi. Mwanamke unakosa lugha tamu kwa mumeo hujui kusema asante, hujui kusema samahani, hujui hata kumsifia mumeo!

Mumeo akikuletea kitu unakipokea na kuamnini ni wajibu wake kukuletea una hiyari ya kusema asante au kukaa kimya. Lakini nataka nikuambie shoga kitu kinacho mtuliza mwanaume ni pamoja na maneno matamu. Mfano amerudi toka kazini baada ya kumpokea lazima umpe pole ya kazi.

“Karibu mpenzi pole na kazi,” akikujibu asante, mwambie.
“Yaani kila muda jicho langu lilikuwa likitazama barabarani utarudi saa ngapi mpenzi wangu,” hata kama ulikuwa ndani ukiendelea na kazi zako.

Vitu hivi humfanya mwanaume kuamini kabisa hata anapokuwa mbali nawe bado ulimuweka moyoni mwako, siyo anakuja baada ya kumpokea unabakia kama bubu haipendezi, tumia ulimi wako kumliwaza mumeo.

Mpo katika safari ya huba mkifika pwani lazima mpeane pole na asante kwa kusafiri salama, pengine wewe umewahi mwenzio naye anakufuata pwani msaidie naye afike pwani na baada ya kufika mpe pole pia kumpa asante kwa kukusafirisha vyema katika bahari ya huba.

Usiwe uvivu wa kuomba msamaha unapokosa, hata kosa lenyewe liwe dogo, kumbuka kosa ni kosa na chanzo cha moto ni cheche. Wapo wachache lugha tamu huzitumia kwa muuza genge ili apunguziwe lakini kwa mumewe vitu hivyo havionekani.Tumia ulimi wako kujenga nyumba yako kumfanya mumeo aone tofauti ya mwanamke wa nje na mkewe ambaye kila neno tamu na zuri humwambia mumewe. Nyama ya ulimi ukiitumia vizuri itakufanya kila siku penzi lako lizidi kuwa tamu, si wajinga waliosema sauti tamu ilimtoa nyoka pangoni na kumtuliza simba mwenye njaa.
Yangu si mengi kwa leo, ila kumbuka wimbo mzuri humbembeleza mtoto akalala.
TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII
KAMA UMEGUSWA NA HABARI ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.
 

KILELE CHA HABARI Copyright © 2014 -- Template created by Mbatta -- Powered by Kilelechahabari