Leo saa tano asubuhi taarifa zilianza kusambaa kuhusu boti ya Kilimanjaro II ikitokea Pemba kwenda Unguja kupata dhoruba ya kupigwa na upepo mkali ilipofika kwenye eneo hatari la Nungwi kulikopelekea sehemu ya mbele ya boti hiyo kuzama kwa dakika kadhaa na kuibuka juu tena.
Kitendo hicho kilipelekea watu ambao idadi yao haijulikani kurushwa kwenye maji kwa sababu walikua wamekaa na wengine wamelala kwenye hii sehemu ambayo ndio ilizama kwenye maji lakini kwenye taarifa iliyotolewa na Polisi on millardayo.com saa saba mchana Jan 5 2014 wakimnukuu Nahodha wa boti hiyo, hakukua na kifo wala mtu yoyote alieachwa baharini.
Tayari mashuhuda na baadhi ya abiria waliokuwemo ndani wameanza kutoa ushuhuda wa vifo na majeruhi ambao waliweza kuogelea au kuokolewa kwenye ajali hii.
Suleiman Masoud ambae yuko msibani Zanzibar kwa sasa, amethibitisha ndugu zake watatu ambao ni watoto wa shangazi yake wamepotea saa kadhaa tu baada ya kutoka Pemba safarini kuelekea Unguja wakiwa na hiyo boti.
Anasema ‘katika waliokwenda kutambua miili kaka mtu pia alikuepo ambapo baada ya kuona maiti ya mdogo wake amezimia mpaka sasa, watoto wa Shangazi ni watatu wamepotea’
‘Jinsi ilivyotokea kwa watoto hawa watatu, walikabidhiwa kwa mama mmoja Pemba ili awatizame kwenye meli ambapo kabla ya boti kufika Nungwi ndani ya boti joto lilizidi hivyo mmoja akawa kapakatwa na huyu mama na wawili ndio wakatoka nje kwenda kupunga upepo ndio wakakutana na hiyo dhoruba wakazolewa na hakuwaona tena kuanzia hapo’
Wakati naipandisha hii stori Suleiman ameniandikia msg inayosema ‘mwili wa mtoto wa pili kati ya watatu waliopotea, umeonekana pia’
Unaweza kumsikiliza Selemani hapa chini pia usisahau kujiunga na mimi kwenye facebook, twitter na instagram kwa jina la Millard Ayo ili uweze kupata kila kinachonifikia hata kama ni saa tisa usiku.
Shuhuda ambae alikua miongoni mwa abiria ndani ya hii boti Mohamed Hamis.
1. Boti ilipofika Nungwi ilizama kwa mbele na mabegi yake na boti ilipokuja juu ikazima na kuzunguka palepale, dakika tano baadae ikawaka ndio tukaondoka watu wakiwa wamebaki kwenye maji.
2. Baada ya boti kuwaka ndio wale watu waliobaki kwenye maji wakatupiwa viokozi vya upepo ndio boti ikaendelea na safari.
3. Hatujui ni watu wangapi waliobaki kwenye maji ila hakuna baharia hata mmoja alieshuka kutoka kwenye boti kwenda kwenye maji.
4. Tulipokaribia bandarini Znz tulitangaziwa kwamba hatutapelekwa bandarini kushuka mpaka tuvue life jacket ili tusionekane nayo manake walitaka habari zisivuje.
5. Wale waliorushwa kwenye maji walichukuliwa na wimbi, watoto na watu wazima nilikua nawaona kabisa wametupwa kwenye maji.
6. Sehemu ya watu walioachwa baharini ni miongoni mwa waliokua wamelala kwenye sehemu iliyozama, kina mama na wengine waliowepesi kutapika ndio ilibidi wakae kwenye hii sehemu ili wapigwe na upepo.
7. Ni ngumu kujua walikua watu wangapi pale mbele kwenye sehemu iliyozama ila ni zaidi ya 20.
Kwa uthibitisho zaidi unaweza kumsikiliza huyu shuhuda hapa chini..