Huu ndiyo muonekano wa dampo hilo la kisasa kwa upande wa juu ambapo ujenzi upo katika hatua za mwishoni.
Chemba
pekee ambayo ni maalum kwa ajili ya kupitishia takataka zenye
kimiminika, pia kupitishia takataka ambazo zitakuwa zimesagwa na
kupelekwa katika bwawa maalum litakalotumika kutengenezea umeme pamoja
na mabaki mengine ya takataka yatatumika kutengenezea mbolea.
Dampo hilo la kisasa kwa ndani ambapo kwa sasa wameweka kokoto ndogondogo chini huku ujenzi ukiendelea.
Hii ni sehemu ya kupaki magari ambayo yatakuwa yakitupa takataka katika dampo hilo la kisasa.
Pichani
ni jinsi takataka kutoka pande mbalimbali za jiji la Mbeya zilivyokuwa
zikitupwa kabla ya dampo hilo la kisasa kujengwa katika eneo hilo jirani
na mlima Nyoka jijini Mbeya. Dampo hilo la kisasa linategemea kuanza
kufanya kazi hivi karibuni.