Mitandao ya ‘Facebook’, ‘Twitter’, ‘BBM’, ‘Instagram’ inafahamika kwa namna inavyoweza kuwaunganisha watu kutokana na urahisi wake katika kuitumia.
Mwananchi Jumapili limebaini kuwa katika mitandao hiyo makundi mbalimbali yameanzishwa yakiwa na malengo tofauti.
Baadhi wameanzisha makundi kwa lengo la kujenga mitandao ya kibishara, kidini, michezo, burudani, vichekesho na mengine ambayo mara nyingi huwa wazi na yeyote anaweza kujiunga na kuona kinachoendelea ndani.
Mbali na hayo ndani ya mtandao wa ‘Facebook na ‘BBM’ yapo makundi yanayoendesha biashara ya ukahaba, yakiwahusisha wanafunzi wa vyuo vikuu mbalimbali nchini.
Uchunguzi umebaini kuwa wanafunzi hao wanaofanya biashara ya ukahaba kwa kutumia mitandao wameweka picha na namba kwa ajili ya mawasiliano kwa mteja atakayekubaliana na bei waliyoweka.
Baadhi ya wanafunzi hao wanatumia mtandao wa ‘University Tanzania Jokes’, ‘Jicho la Mvulana Liko Fasta Kuliko Google’, ‘Benki ya Utamu Tanzania’ na nyingine katika kufanikisha biashara hiyo ya ngono.
Ukiingia katika mitandao ya Facebook, Twitter, BBM, Instagram, utabaini kuwapo kwa makundi yaliyoundwa kutengeneza mitandao ya ngono, ambayo huweka pia namba za simu za wahusika, zikiambatana na picha, ambao ikiwa utaangalia picha na kuvutiwa, unaweza ukapiga simu husika kuzungumza naye kwa kufanya mapatano kabla ya kukubaliana.
Uchunguzi wetu umebaini kuwa mwanamume anaweza kumpata msichana kutoka chuo kikuu chochote nchini anayefanya biashara ya ukahaba kupitia mitandao hiyo.
Baadhi ya vyuo wanavyotoka wasichana wanaofanya biashara hiyo na kujitangaza kwenye mitandao ni pamoja na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine (SAUT), Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) na Chuo cha Usimamizi wa Fedha
-Mwananchi