Blandina Chagula ‘Johari’.
Tukio hilo lilitokea wikiendi iliyopita katika Viwanja vya Leaders
Club, Kinondoni, Dar ambapo uchaguzi wa safu mpya ya uongozi wa klabu
hiyo ulimalizika na matokeo kuwatangaza mwenyekiti mpya Steven Mengele
‘Nyerere’ na wenzake kuwa washindi.Katika mahojiano na mwandishi wetu, Johari alisema: “Kwa upande wangu ninawaamini viongozi wote waliochaguliwa katika kutuletea maendeleo katika klabu yetu kwa kufanya kazi kwa umoja na mshikamano. Wote nawaamini na kusema kweli, hawa ndiyo viongozi tuliokuwa tunawataka.”
Katika uchaguzi huo, nafasi ya Makamu Mwenyekiti ilikwenda kwa Mahsein Awadh ‘Dk. Cheni’, Katibu Mkuu Willium Mtitu, Katibu Msaidizi Devotha Mbaga, Mweka Hazina Issa Mussa ‘Cloud’ na msaidizi wake Sabrina Rupia ‘Cathy’.