 
Shuhuda Abdul Ally ambae ni mkuu wa 
nyumba zilizokaribu na alikopigwa  Mwenyekiti huyu, anasema walisikia 
kelele za huyu mtu kupigwa saa tisa  usiku na walipomsogelea walimkuta 
peke yake.
‘Niliomba wasiniue, wamenipiga sana… 
wamenichukua saa tano nyumbani  kwangu Kwa Aziz Ally, wao walikua na 
gari kama ya Polisi lakini  inaonekana sio ya polisi wakasema 
tunakupeleka Central, tulikua wanne na  hawakuhangaika na mtu 
wakanichukua mimi moja kwa moja.. tulipopanda  kwenye gari wakachukua 
nguo yangu wakanifunga uso, wakaanza kunipiga  wakisema nisiwajibu na 
hawakuniambia chochote’












 
 
 
 
 
 
