Ama kweli wadada wa mjini wana mambo
sana, wenyewe wanasema kua mjini shule kijijini kilimo. Sasa huku kuja
kwa mitandao ya jamii kumeibua makubwa ambayo tulikua hatuyajui. Mwanzo
Facebook ilikua ndo kila kitu kwa umbea wote wa town unaupata kule ila
kwa sasa mambo yamebadilika kabisa, Insta ndo habari ya mjini. Kila
kitu utakipata Insta hadi madalali lol.
Sasa habari tulizozipata kutoka huko
huko insta ni kua baada ya Raisi wa wasafi bwana Diamond au Halima
Kimwana anavyopenda kumwita Chibu Dangote kutemana na mwanadada
DvjPenny na tetesi kusema kua Diamond wamerudiana na wema hili
tulilolinasa laweza kuwashangaza wengi sana
Habari zilizotafutwa na mdakuzi wa
vitukovyamtaa kupitia mtandao mmoja maarufu zinasema kua Bwana Diamond
ana mtoto mpyaaa tena mkali ile mbaya. Katika pitapita yetu Insta
tukakutana na post ya mtu mmoja hivi ambaye kila kukicha yeye ni
kumtetea aliyekua X wa Diamond mwanadada Penny. Post hiyo iliandikwa "Uwiiiiii
chaggabarbie aijasimama Bado hapo au nayo kibamia kwako ivi nimuulize
diamondplatnum nae anayo kama hiyo nn eti wemasepetu vjpenny04 mana
mnatoana macho kwa mtoto wa tandale sasaivi nasikia anapumzika kwa
hamisa mobeto wanafata hii Kitu Kina dada tuambizane na dai nae anayo
nini kama anayo ukitoka kwa hamisa nenda zamu chagga Basi uwiiiiii chaga
una balaa ww Kitu na box ndomambo yako chagga be like keep calm its
just a big di**"
Sifa kubwa ya mwenye hiyo akaunti ni
kumtetea sana Penny na nahisi atakua ni mtu wake wa karibu kwani kuna
vitu vingine anaandika ni vigumu kwa mtu ambaye si wa karibu na Penny
kuvijua. Waswahili wanasema kua lisemwalo lipo na kama halipo basi
laja, Je ni kweli Bwana Diamond anatoka na mtoto mzuri Hamisa?????
Swali linabaki hapo???
Lakini kama utakua mfatiliaji mzuri wa
mastory haya utakumbuka kua karibu mademu wote waliotembea na Diamond
na baadae kujulikana ilianza kama tetesi hivi hivi, mfano mzuri ni
Wema, Yule aliyekua demu wa Mr Blue, Penny, Jokate na wengine ambao ni
ngumu kuwataja.
Kwa wale msiomjua Hamisa ni nani, ngoja
niwape profile yake kwa ufupi tu. Hamisa ni Model. Umaarufu wake
umeongezeka sana siku za hivi karibuni kwani kuna makampuni mengi
yanamtafuta kufanya matangazo nae kutokana na uzuri alionao. Kwa wale
mlibahatika kuliona Jarida la Pulse Kenya mwezi huu mwanadada Hamisa
ndo alipamba ukurasa wa mbele.
Kama ni kweli Bwana Diamond kaamua
kujituliza kwa Hamisa itakua poa coz mtoto kasimama kila idara, Unaweza
tazama picha za mwanadada Hamisa zilizokusanywa na mdakuzi wa
Vitukovyamtaa hapa chini.