VIJANA watatu wa familia moja ya
Felipe Ramirez, wamepata balaa kubwa baada ya kuota matiti
yaliyosababisha kuchekwa na vijana wenzao waliokuwa wakiwaona kuwa ni
mashoga.
Vijana hao kutoka katika Jamhuri ya Dominica ni Yeuri (17 ), Gabriel (11) na Daniu Ramírez (12), hata hivyo, kwa sasa wanaishi kwa amani baada ya kufanyiwa upasuaji na kuondolewa matiti hayo.
Vijana hao kutoka katika Jamhuri ya Dominica ni Yeuri (17 ), Gabriel (11) na Daniu Ramírez (12), hata hivyo, kwa sasa wanaishi kwa amani baada ya kufanyiwa upasuaji na kuondolewa matiti hayo.
Baba yao mzazi, Felipe Ramirez
alifanya jitihada ya kuomba msaada kupitia televisheni na magazeti ili
wanawe wafanyiwe upasuaji kwani walikuwa wakiishi katika mateso kwenye
jamii yao.
Baada ya kuomba msaada, Mkurugenzi wa
Hospitali ya Marcelino Velez Santana nchini humo, Dokta Pedro Antonio
Delgado aliamua kuwalipia gharama za upasuaji ambao ulichukua saa
mbili.
Ramirez, alisema: “Wakati wanaingizwa
katika chumba cha upasuaji nilikosa raha kwa kuhofia kama watatoka
salama nao waliogopa lakini baada ya kutoka, wote tumefurahi sana.”