Ofisa Elimu Msingi, Wilaya ya Nkasi, Bw. Misana Kwangura akizungumza na Thehabari.
Aidha
aliongeza kuwa kwa mwaka 2011 jumla ya wanafunzi 16 wa shule za msingi
walitiwa mimba na kukatizwa masomo yao. “…Kimsingi naweza kusema matukio
haya kwa sasa yanapungua ukilinganisha na hapo nyuma, na hii inatokana
na elimu ambayo tunaitoa kwa kuzunguka kwenye shule mbalimbali kwa
kutumia ofisi ya Ofisa Elimu Sayansi Kimu,” alisema Kwangura