
Mfanyabiashara wa madini aliyefahamika kwa jina moja la Jimmy amejikuta katika wakati mgumu baada ya kufumaniwa na mkewe akiwa na kimada gesti.
 Tukio hilo lililofunga mtaa kwa kujaza wambea kibao, lilitokea hivi 
karibuni ndani ya gesti moja  Kinondoni jijini Dar es 
salaam ambapo mke wa mfanyabiashara huyo (jina halikupatikana mara 
moja), alimnasa mumewe  akijiandaa kuvunja amri ya sita ya Muumba.
Wadakuzi waliokuwa eneo la balaa walitonya kuwa, siku hiyo ya tukio, Jimmy ambaye ni mkazi wa jijini Arusha, alifika Dar kibiashara na baadaye alimsaka kimada huyo wa siku nyingi na kwenda kujirusha naye bila kujua mkewe alishatonywa juu ya usaliti wake.
Jimmy kabla ya kuingia gesti inadaiwa 
alijipumzisha katika grosari iliyo karibu na Mango Garden Bar, baadaye 
akaenda kwenye gesti hiyo ya jirani bila kujua mkewe alikuwa akitua mguu
 kila pale yeye aliponyanyua, akazama ndani ya gesti hiyo na kuanza 
kujiandaa kwa zinaa.

Jimmy alikutwa tayari ameshavua nguo zote na kubakiwa na ‘boksa’ huku kimada naye akiwa na ‘kufuli’ pekee.
Kilichofuata hapo ni kipigo, mke wa Jimmy alianza kumtembezea kipigo 
yule kimada. Waandishi nao walivamia na kutandika picha za timbwili ambapo 
Jimmy alifanikiwa kupenya mlangoni na kukimbia bila kujali nguo 
nyingine.
Kutokana na kelele za timbwili hilo, majirani wa eneo hilo
 walifika kuhoji kulikoni ambapo mfumaniaji huyo alitoboa siri kwamba 
amekuwa akimfuatilia mumewe kwa siku nyingi baada ya kuambiwa ana kimada
 Dar.
Wakati pakichimbika, kimada huyo alisikika akimlaumu Jimmy kwamba 
amemuingiza kwenye mkenge akijua mkewe ni mdodosaji wa mambo na anaweza 
kufika Dar madai ambayo hayakuwa na wa kuyajibu.


 
 
 
 
 
 
