Like Us On Facebook

HUU NI UKATILI:DENTI ABAKWA, APIGWA MIMBA NA KUTOROKA KWAO...MSHITAKIWA AMFUKUZA KAMA MBWA AKIWA NA MTOTO MCHANGA

MWANAFUNZI wa kidato cha tatu katika shule ya Bujingwa, iliyopo Nyakato Mwanza (jina linahifadhiwa), mkazi wa Mabatini jijini Mwanza, alibakwa, kutoroshwa nyumbani kwao na hatimaye kupewa mimba na mtu aliyefahamika kwa jina la Roja (27).

Denti huyo akiwa na mwanaye.
 
Akizungumza na gazeti hili hivi karibuni jijini Mwanza akiwa hoi kimaisha baada ya kufukuzwa kwa mwanaume huyo, denti huyo ambaye sasa ana mtoto mwenye umri wa miezi saba, alisema baada ya kutoroshwa kwao, mwanaume huyo alimpa mateso mengi, ikiwa ni pamoja na vipigo vya mara kwa mara.
Mtuhumiwa aitwaye Roja.

Akisimulia kwa masikitiko, alidai kuwa Roja alimpa mimba akiwa bado mwanafunzi wa  kidato cha tatu mwaka 2012 na kumshawishi atoroke nyumbani kwao ili akaishi naye.
Alidai kuwa, usiku wa Desemba 9 mwaka huu, Roja akiwa na baba, alifika nyumbani na kumtaka aondoke mara moja huku akimtupia virago vyake nje ya nyumba bila kujali kuwa na kitoto kichanga.
Hati ya makubalianao.

Siku hiyo alifika nyumbani na kunitaka niondoke , nilipokataa akaanza kunipiga na chuma kichwani na kunikaba shingoni bila kujali nilikuwa na mtoto mgongoni. Nilipoona hali inazidi kuwa mbaya nikaamua kuondoka zangu na kuja hapa ili nisaidiwe,” alisema mwanafunzi huyo ambaye wakati huo alikuwa katika ofisi za taasisi inayojishughulisha na utetezi wa haki za binadamu iitwayo Farijika.
Katika kuchimba ukweli wa madai hayo, Oparesheni Fichua Maovu (OFM) ilizungumza na wazazi wa denti huyo ambao  kwa muda tofauti walikiri taarifa za mtoto wao kutoroshwa na kubakwa hadi kuzalishwa na mwanaume huyo.
PF3.
Kuhusu manyanyaso anayopata mtoto wao, walisema anastahili  matibabu (PF3) ambapo vipimo vilionesha kuwa kweli alifanyiwa vitendo hivyo kwa kuwa alikuwa na majeraha ya ndani kwa ndani.
Baada ya kuthibitisha hilo, Roja aliitwa mbele ya watetea haki hao na kukiri kumnyanyasa mkewe lakini akiahidi kutomnyanyasa tena kabla ya kusaini hati ya makubaliano iliyoshuhudiwa na mashahidi watatu, hati ambayo kama akiivunja atafikishwa mahakamani kwa makosa mbalimbali ikiwemo kubaka na shambulio la mwili.
Mama na mtoto wanaonyanyaswa na kijana Roja.

CREDIT: GPL

TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII
KAMA UMEGUSWA NA HABARI ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.
 

KILELE CHA HABARI Copyright © 2014 -- Template created by Mbatta -- Powered by Kilelechahabari