Like Us On Facebook

YULE SHABIKI WA YANGA BINGWA WA KULIA AJITOSA BONGO MOVIE,APEWA SCENE YA KULIA,MTAZAME HAPA AKIMWAGA CHOZI


Shabiki maarufu wa Yanga Steven amejitosa katika fani ya filamu ambapo ataanza kuonekana karibuni akiwa katika muvi inayoandaliwa na Dr Cheni itayokwenda kwa jina la 'Nimekubali Kuolewa'. 
 
Steven alijipatia umaarufu ghafla baada ya mitandao kurusha video inayomwonesha analia baada ya timu ya Yanga anayoishabikia kufungwa. 

Kwa upande wa Dr Cheni ambaye ni msanii aliyeanza fani hii takriban miaka 15 iliyopita, anakuja kiviungine baada ya kukaa kando kwa mwaka mmoja.

Katika filamu hii pia kuna nyota kutoka China ambaye anakuwa Mchina wa kwanza kuigiza kwenye Bongo Movie.
 
Tazama moja ya scene ya filamu hiyo jamaa akimwaga chozi kama kawaida
TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII
KAMA UMEGUSWA NA HABARI ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.
 

KILELE CHA HABARI Copyright © 2014 -- Template created by Mbatta -- Powered by Kilelechahabari