Nimesikia
watu wengi mno wakilalamika kuwa matumizi ya Kiingereza kingi kwenye
show yake yamewafanya wasikipende kipindi hicho na kunifanya nihoji,
nani walengwa hasa wa kipindi chake? Kwa niaba yao ningependa
kulifikisha ombi lao kwa Wema kuwa atumie zaidi Kiswahili katika kuongea
ili wengi wamwelewe.
Pamoja
na kwamba Wema ndivyo alivyo na hata wakati akihojiwa kwenye TV/RADIO
ndivyo huongea, ajizuie katika kipindi chake ili kila mtu amfuatilie.
Katika elimu yangu ya uandishi wa habari na utangazaji wa radio/TV nilifundishwa kuwa, wakati wa kuandaa kipindi chochote kile, ni lazima ubainishe, walengwa wa kipindi chako (target audience).
Kwa
kuangalia umaarufu wa Wema Sepetu, hakuna shaka kuwa walengwa wake
wakubwa, ni watu wa kawaida kabisa ambao ndio wanunuaji wakubwa wa
magazeti ya udaku yaliyolikuza jina lake nchini na wamekuwa wakimpenda
sana.
Kwa namna anavyokiendesha kipindi chake kwa kusimulia matukio yanayooneshwa kwenye kipindi, walengwa ni wale wanaokielewa Kiingereza. Swali ni je, wasomi, raia wa kigeni au watoto wa Masaki, Osterbay na maeneo mengine ya watu wa hali ya juu wanaosoma ama waliosoma kwenye shule za kishua wanakiangalia kipindi hicho? Sio kweli na kama wapo basi ni wachache.
Watu
kama hao kwanza hawatumii ving’amuzi vinavyotumika na watu wa hali ya
kawaida ambako TV za kibongo zipo. Watu wa maeneo hayo, huangalia DSTV
zaidi ambako huko hupenda kuangalia vipindi vya kinyamwezi kama, Keeping
Up With the Kardashians, Ice Loves Coco, The Hustle Family ya T.I na
Tiny ama The Real Husbands of Hollywood na zingine kibao.
TV
za kibongo huangaliwa kwa nadra na tena labda wakati wa taarifa ya
habari saa 2 usiku, na baada hapo huendelea kuangalia TV za nje.
Kipindi cha Wema Sepetu ambacho huoneshwa na runinga ya EATV, kinaangaliwa zaidi na watu wa kawaida ambao kwa bahati mbaya amekuwa akiwatenga kwa kupenda mno kuongea Kiingereza.
Kipindi cha Wema Sepetu ambacho huoneshwa na runinga ya EATV, kinaangaliwa zaidi na watu wa kawaida ambao kwa bahati mbaya amekuwa akiwatenga kwa kupenda mno kuongea Kiingereza.
Tanzania
bado hatujafika huko na hilo Wema anapaswa aliweke kichwani mwake.
Asiletee maisha ya Hollywood kwenye kipindi kinachoangaliwa na Mtanzania
wa kawaida.
Kama angekuwa hajui kabisa Kiswahili, basi hilo lingeeleweka. Abadilike..
Kama angekuwa hajui kabisa Kiswahili, basi hilo lingeeleweka. Abadilike..