Like Us On Facebook

SHILOLE KUWAPELEKESHA MADEE, CHEGGE BILLS....SOMA ZAIDI HAPA

WASANII wa muziki wa kizazi kipya Bongo, Hamad Ally ‘Madee’ na Juma Saidi ‘Chege’ wikiend hii watazindua video (vichupa) za nyimbo zao mpya ndani ya Ukumbi wa Club Bilicanas, jijini Dar es Salaam.


 

Zuwena Mohamed ‘Shilole’.

Akizungumza na gazeti hili juzikati, ‘Rais wa Manzese’ Madee alisema katika shughuli hiyo watasindikizwa na mkali wa kibao cha Nakomaa na Jiji, Zuwena Mohamed ‘Shilole’.

 

Hamad Ally ‘Madee.

“Mimi nitatoa video ya wimbo wangu mpya wa Tema Mate Tuwachape ambao nimeufanya na Studio ya Ogopa Djs wa Kenya na Chegge yeye atakuwa na video ya kibao chake cha Ubinadamu ambao pia ameufanyia Ogopa,” alisema Madee.

Alisema siku hiyo (Jumapili hii) kutakuwa na red carpet ambapo mashabiki watapiga picha na mastaa wao huku Chegge pia akizindua mtandao wake (Web site).
-GPL

TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII
KAMA UMEGUSWA NA HABARI ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.
 

KILELE CHA HABARI Copyright © 2014 -- Template created by Mbatta -- Powered by Kilelechahabari