BAADA ya hivi karibuni staa wa filamu Bongo, Ruth Suka ‘Mainda’ kueleza mazito kuhusu Ray, Johari na Chuchu Hans, msanii mwenzake, Nuru Nassoro ‘Nora’ naye amefunguka kuwa laana ya walichomfanyia miaka ya nyuma itawatesa Ray na Johari mpaka kifo chao.
Akizungumza na GPL, Nora alisema Ray na
Johari walimfanyia ‘mambo mabaya’ yaliyosababisha kupotea kabisa kwenye
sanaa ya filamu hadi alipoibuka upya hivi karibuni.
“Kinachowasumbua Ray na Johari ni laana yangu na kweli nimeamini
Mungu analipa hapahapa duniani kwani walinifanyia mambo ya ajabu,
wakanipoteza kabisa kwenye fani, walinifanya nichanganyikiwe wakijua
sitapona, lakini sasa hawaelewani tena wakati walikuwa wanapendana kama
pete na kidole.
“Nakumbuka zamani nilikuwa nikishonea nywele nzuri lazima Ray naye
akamnunulia Johari kama hizo za kwangu, alimtengeneza Johari akawa
anaigiza kama mimi na kujifanya yeye ndiyo mimi mpaka waliponipoteza
kwenye fani.
“Namshukuru Mungu nimejikongoja na hatimaye nimerudi tena kwenye
sanaa, mabaya waliyokuwa wakinifanyia yamewarudia wenyewe, jamani
mwacheni Mungu aitwe Mungu kwani nakesha nikiomba na ninaamini maadui
zangu wote wataumbuka mchana kweupe,” alisema Nora.
-GPL
-GPL