Wananchi wakishuhudia mwili wa mtu aliyetuhumiwa kuiba pikipiki ukiteketea kwa moto |
Polisi wakiondoka na mwili wa marehemu
MTU
mmoja asiyefahamika jina wala makazi yake, amepoteza maisha baada ya
kupigwa na kuchomwa moto na wananchi ambao wameamua kujichukulia sheria
mkononi.
Wananchi hao ambao ni wakazi wa eneo la Mtakuja Mbalizi, walifanya tukio hilo jana majira ya saa mbili asubuhi.
Mwenyekiti
wa Kijiji cha Mtakuja Mbalizi Mbeya vijijini, Ambonisye Masinga, alisema
kuwa marehemu huyo alidaiwa kuiba pikipiki eneo la Utengule.
Alisema,
baadhi ya madereva wa bodaboda(pikipiki) walianzisha msako na kufanikiwa
kumtia nguvuni marehemu huyo na kuanza kumshushia kipigo huku
mwili wake ukiwa umefungwa kwenye pikipiki na kuuburuza barabarani
umbali wa kilomita moja.
Alisema,
mwili huo uliburuzwa na kufikishwa kwenye eneo la mlima reli maarufu kwa
jina la eneo la adhabu kwa wahalifu na kuchoma moto mwili wake.
Aidha,
katika tukio hilo fundi ujenzi aliyekuwa katika eneo hilo Asangalwisye
Mayasu(50) mkazi wa kivukoni, alijikuta akiambulia kipigo baada ya
kujaribu kuwazuia wananchi ambao waliamua kujichukulia sheria mkononi.
“Baada
ya msamalia huyu kupigwa na kuumizwa vibaya serikali ya kijiji
ilimkimbiza hospitali Teule ya ifisi na kwamba hali ya afya yake si
nzuri hali iliyopelekea mke wake aitwaye Kristina Kyando (45)
Kuzirai,”alisema
Hata
hivyo Kamanda wa Polisi mkoa wa Mbeya, Diwani Athumani, alithibitisha
kutokea kwa tukio hilo na kwamba jeshi la polisi litahakikisha linawatia
mbaroni watu wote waliohusika na mauaji hayo.
Kumeibuka
kwa vitendo vya madereva pikipiki kujichukulia sheria mkononi ambapo
hivi karibuni walifunga barabara ya Iwambi Jijini Mbeya kwa
kulishinikiza jeshi la polisi kuwaachia watuhumiwa wawili ambao
walituhumiwa kuiba pikipiki ili wawaue.
|