Ayubu Mnazi Alphonce(24) ni kijana ambaye amelazwa katika hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Tabora Kitete akipatiwa matibabu baada ya kuamua kuukata uume wake kwa kutumia wembe mpya ili kuepukana na usumbufu anaoupata kutoka kwa wanawake ambao amekuwa nao kimapenzi...
Imeelezwa kuwa baada ya kutokea mfarakano baina yake na mwanamke mmoja
ambaye jina lake halijafahamika,Ayoub aliamua kuingia ndani na kuukata uume wake
kwa kutumia wembe mkali na kisha kuutupa
nje..
Taarifa
kutoka Jeshi la Polisi zinaeleza kuwa baba mzazi wa Ayubu baada ya
kubaini kuwa mtoto wake alikuwa amejifungia chumbani kwa muda mrefu, aliamua
kumgongea mlango na alipopata fursa ya kuingia ndani ndipo alipogundua
ukweli juu ya jambo hilo na hivyo kumpeleka Ayubu Kituo kikubwa cha
Polisi Tabora ambapo jalada la kesi ya kujidhuru lilifunguliwa.
Hata
hivyo hali ya Ayubu kwasasa inaendelea vizuri licha ya kuwa amejikata
na kubakisha kipande cha sentimeta 5 huku akisubiriwa kufikishwa
mahakamani kwa kutenda kosa hilo la kujidhuru mwenyewe pasipo sababu za
msingi.