NAIBU Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mwigulu Nchemba,
amemchambua mwanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)
na kusema kuwa ni mchanga kwenye siasa hivyo hamuogopi.
Hatua hiyo ya Mwigulu imekuja baada ya mwishoni mwa wiki iliyopita, Dk. Kitila kumshangaa mbunge huyo wa Iramba Magharibi, kuwa amejifanya kumwonea huruma katika kipindi hiki ambacho amevuliwa wadhifa wake wakati hapo awali alikuwa akimponda.
Kutokana na hali hiyo, Nchemba alimtupia vijembe, Dk. Mkumbo ambaye alikuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, na kusema kuwa hana hofu kutokana na lengo lake la kulitaka jimbo hilo.
Mwigulu, alisema ana uhakika wananchi wa jimbo hilo wanamwamini na wataendelea kumwamini kwani yeye ni mbunge wa kwanza kuleta mabadiliko makubwa ndani ya jimbo hilo.
Nchemba alisema kwa kuwa Dk. Kitila ni mwanasiasa mchanga kwake, anapaswa kuendelea kukua kisiasa na ndiyo maana amekuwa mstari wa mbele kumtetea na kumuhurumia pale anapoonewa.
Alisema maneno ya Dk. Mkumbo, yanatokana na tofauti zao kisiasa, kichama na kimtazamo, lakini yeye kama mwanasiasa kijana, anapenda kuona vijana wenzake wakipiga hatua.
Hivi karibuni, Dk. Mkumbo alisema kwamba Mwigulu anapaswa kukaa mbali na kuacha kimbelembele cha kumsifia na kwamba atahakikisha analichukua jimbo la Iramba Magharibi.
“Mwigulu Nchemba amekuwa akinichafua, lakini tangu nivuliwe nafasi yangu ndani ya chama amejifanya kunisifu na kunihurumia.
“Kutokana na hali hiyo, namuonya na kumwambia mvua inyeshe jua liwake ni lazima nitamvaa katika uchaguzi wa Ubunge kwenye uchaguzi mkuu ujao,” alisema Dk. Kitila.