Like Us On Facebook

MPIGA DEBE AUAWA WAKATI AKIGOMBANIA Tshs. 1,000 (BUKU) NA WENZAKE..


NI jambo la kusikitisha kweli.
Kijana mmoja aliyefahamika kwa jina la Komba Faustine Aloyce ambaye ni mpiga debe, amefariki dunia baada ya kugongwa na gari wakati akipigana na mwenzake katikati ya barabara wakigombea shilingi elfu moja waliyopewa kama ujira katika kituo cha daladala kilichopo Kasanga nje kidogo ya Manispaa ya Morogoro.

Mwili wa mpiga debe, Komba Faustine Aloyce ukifunikwa kabla ya kutolewa eneo la ajali.
Tukio hilo la kusikitisha lilitokea Jumamosi iliyopita kwenye kituo hicho cha daladala zitokazo Mzumbe, Mlali, Mgeta Melela, Doman na Morogoro mjini kilichopo kando kando ya Barabara Kuu ya Morogoro-lringa.
Mashuhuda wa tukio hilo walililiambia gazeti hili kwamba Komba na mwenzake huyo aliyefahamika kwa jina moja la Alunaki, waligombea fedha hiyo waliyopewa baada ya kufanya kupiga debe ambapo kila mmoja alidai ilikuwa yake.
...Ukiingizwa kwenye difenda ya polisi.
Wakati wakiendelea kupigana, gari moja lilitokea kwa kasi, Alunaki aliwahi kukimbia lakini bahati mbaya Komba akakanyagwa na kufariki papo hapo. Kabla ya kupigana, inadaiwa wawili hao walizozana kwa muda mrefu.
Dada wa marehemu, Mary Osward alisema mdogo wake huyo alifika na kuishi nyumbani kwake tokea mwaka jana akitokea Kilosa na kwamba kupiga debe ndiyo ilikuwa kazi yake.
Baadhi ya wananchi waliofika kushuhudia tukio hilo.
“Mdogo wangu alikunywa chai kisha akaniaga anaelekea kazini kwake, lakini baada ya muda nikaona watu wanakimbilia barabarani nilipowauliza kuna nini wakaniambia mdogo wangu amegongwa na gari, nilipofika nikamkuta ndiyo anakata roho,” alisema kwa masikitiko dada huyo.

- GPL
TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII
KAMA UMEGUSWA NA HABARI ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.
 

KILELE CHA HABARI Copyright © 2014 -- Template created by Mbatta -- Powered by Kilelechahabari